• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bandari ya Tanga sasa kupunguza foleni Dar

    (GMT+08:00) 2015-07-22 19:36:31

    Msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, unatarajiwa kupungua kwa asilimia 4 baada ya Serikali kufanya uamuzi wa kuruhusu uingizaji wa shehena ya mafuta nchini kupitia Bandari ya Tanga.

    Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uagizaji na Usimamiaji Mafuta (PIC), Michael Mjinja anatoa taarifa hii.

    Meli ya mafuta ya Ardmore Sea mariner ilipokewa na watendaji wakuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Ewura, wafanyabiashara ya mafuta, viongozi wa dini, Serikali vyama vya siasa na wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta nchini na kupakua shehena ya tani 20,500 ya mafuta ya dizeli na petroli.

    Anasema manufaa ya kiuchumi yatakayopatikana kutokana na kupitishia shehena ya mafuta ni kupungua kwa masongamano wa magari jijini Dar es Salaam kwa kati ya asilimia tatu na nne, lakini pia uchumi wa Mkoa wa Tanga utainuka.

    Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga, Swalehe Byarugaba anasema kupitia shehena hiyo ya mafuta, wanatarajia kukusanya kodi ya Sh bilioni 11 mwezi Julai.

    Awali, makusanyo ya TRA mkoani Tanga yalikuwa Sh bilioni 5 kwa mwezi wakati ikikusanya kodi kupitia Shehena Kavu (Dry Cargo) pekee.

    Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga, Henry Arika anasema kuwasili kwa meli hiyo kunatokana na Serikali kupitisha uamuzi wa kuifanya Bandari ya Tanga kuwa ya pili kwa upokeaji mafuta baada ya Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako