• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la Taliban lathibitisha kifo cha Mullah Mohammad Omar

    (GMT+08:00) 2015-07-31 10:51:35

    Kundi la Taliban jana usiku lilitoa taarifa likithibitisha kuwa kiongozi wake Mullah Mohammad Omar alifariki dunia kwa ugonjwa, lakini halijadokeza muda na sehemu alipokufa.

    Wizara ya mambo ya nje ya Pakistan inasema kutokana na kifo chake cha Omar, duru ya pili ya mazungumzo ya amani ya Afghanistan iliyopangwa kufanyika leo nchini Pakistan imeahirishwa.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang jana alisema China inaelewa kuahirishwa kwa mazungumzo hayo. Amesema China inazitaka pande husika kutupia macho umoja na amani ya kudumu ya Afghanistan, kuendelea kuhimiza mchakato wa amani na usuluhishi ambao unalingana na maslahi ya watu wa Afghanistan na pande mbalimbali, amani na utulivu wa sehemu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako