• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yaongeza ulinzi wa Eurotunnel ili kukabiliana na wahamiaji haramu

    (GMT+08:00) 2015-07-31 16:57:57

    Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Theresa May ameahidi kuchukua hatua zaidi za dharura ili kuzuia maelfu ya wahamiaji haramu kuingia nchini humo kupitia njia ya Eurotunnel.

    May amesema hayo alipoongoza kikao cha serikali kujadili suala hilo baada ya ripoti kuwa mtu mmoja amefariki jumanne wiki hii wakati wahamiaji haramu 1,500 walipojaribu kuingia kwenye njia hiyo kutoka mji wa Calais, kaskazini mwa ufaransa. Amesema wahamiaji wengi wamejaribu kuingia nchini Uingereza kupitia Eurotunnel kabla ya uzio wa eneo hilo kuimarishwa.

    May amesema, jambo la muhimu kwa sasa ni kutafuta njia za kuimarisha usalama katika njia ya reli ya Coquelles, ili kuhakikisha kuwa wahamiaji hao hawataingia nchini Uingereza kupitia Eurotunnel

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako