• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yachunguza dai la daktari wa nchi hiyo kuua Simba nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2015-07-31 17:04:59

    Ikulu ya Marekani imesema itapitia upya ombi la umma la kumrejesha nchini Marekani Walter Palmer aliyeua Simba kinyume na sheria nchini Zimbabwe.

    Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bw. Josh Earnest amesema hatua hiyo itaamuliwa na jinsi Wizara ya Sheria ya nchi hiyo inavyoshughulikia utaratibu wa kumrejesha kwenye nchi aliyofanya kosa. Amesema:

    "Kitakachofanyika ni kwamba kutakuwa na mchakato ambao Ikulu itatoa majibu kwa malalamiko juu ya mauaji hayo. Msingi ni kwamba mtu yeyote anaweza kufungua tovuti ya Ikulu na kutoa ombi lake, na kama watu laki moja watasaini ombi hilo katika muda uliopangwa ambao ni siku 30 au 60, basi watapata jibu rasmi kutoka mamlaka husika. Inaonekana kuwa kama ombi hilo limefikia kiwango kinachohitajika, na kutakuwa na jibu kutoka Ikulu. Kwa ujumla maamuzi ya kufungua mashtaka ama kumrejesha mtu huyo kwenye nchi aliyofanya makosa yatafanywa na Wizara ya Sheria."

    Palmer ambaye ni daktari wa meno kutoka Minneapolis amekubali kuwa amemuua Simba aitwaye Cecil ambaye alikuwa kivutio kikubwa cha utalii katika hifadhi ya taifa ya Hwange nchini Zimbabwe. Uchunguzi wa kesi hiyo utafanywa na Shirika la Huduma za Wanyamapori na Samaki la Marekani ili kuchunguza kama alivunja sheria ya Marekani ya kujihusisha na biashara haramu ya wanyama pori.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako