• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukweli wa wimbi la kupungua kwa wawekezaji wa kigeni nchini China

    (GMT+08:00) 2015-08-12 16:39:43






    Ripoti kuhusu uwekezaji wa dunia iliyotolewa hivi karibuni kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa biashara na maendeleo inasema, thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja duniani kwa mwaka jana imefikia dola za kimarekani trilioni 1.23, ambayo imepungua kwa asilimia 16 kuliko mwaka 2013, na hiyo inatokana na kufufuka taratibu kwa uchumi wa dunia na migogoro ya kisiasa kwenye baadhi ya nchi. Ripoti hiyo imesema China imevutia uwekezaji wa dola za kimarekani bilioni 129 kutoka nchi za nje, ikichukua nafasi ya Marekani na kuwa nchi inayovutia uwekezaji wa nje kwa wingi zaidi duniani.

    Wakati huo huo, vyombo vingi vya habari vinasema hivi sasa idadi kubwa ya wawekezaji kutoka nje wanaondoka nchini China, na kwamba viwanda vingi vya nchi za nje nchini China vimefungwa, huku wawekezaji hao wakihamia nchi za Asia Kusini Mashariki ambapo gharama za ardhi na nguvukazi ni chini zaidi, au wawekezaji wamerudi kwenye nchi zao. Kwa mfano, kampuni ya utengenezaji wa saa ya Citizen ya Japan mwezi Februani mwaka huu ilitangaza kufunga kiwanda chake mjini Guangzhou, Microsoft inapanga kufunga viwanda vya kutengeneza simu za mkononi vilivyoko mijini Dongguan na Beijing, na inaharakisha hatua za kuhamisha zana za utengenezaji nchini Vietnam.

    Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, idadi ya kampuni mpya zilizoanzishwa na wawekezaji wa nje kwenye robo ya kwanza ya mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 22.4, huku thamani ya matumizi halisi ya mitaji ya kigeni ikiongezeka kwa aslimia 11.3. Wakati huo huo, idadi ya kampuni zilizofungwa imepungua kwa asilimia 17.6 kuliko mwaka jana wakati kama huu, na idadi ya kampuni zilizopunguza uwekezaji imepungua kwa asilimia 35.7. Kuhusu kufungwa kwa baadhi ya kampuni za nje nchini China, mkurugenzi wa idara ya biashara kwa nje iliyo chini ya wizara ya biashara ya China Bw. Tang Wenhong amesema,

    "Athari zinazotokana na kufungwa kwa kampuni za nje kihalisi ni ndogo, sio viwanda vingi vya kigeni vya utengenezaji vimeondoka nchini China mpaka hivi sasa."

    Takwimu husika zinaonesha kuwa, mwaka jana kwa ujumla viwanda vikubwa vyenye uwekezaji wa nje vilivyo na mapato zaidi ya yuan milioni 20 kwa mwaka vilipata faida ya yuan trilioni 1.6, ambayo imeongezeka kwa asilimia 9.5 kuliko mwaka 2013, na kuzidi kiwango cha wastani nchini China kwa asilimia 6. Kati ya kampuni za nje zilizoko katika nafasi 1000 za mbele kwa mapato katika mwaka 2010, kampuni mbili tu zimefungwa kutokana na uendeshaji mbaya, nyingine 10 zimebadili na kuwa kampuni ya uwekezaji wa ndani kwa kupitia kuhamisha hisa, hali ambayo haikuleta athari yoyote kwa ajira na uzalishaji katika viwanda hivyo. Kwa upande wa ukubwa wa uwekezaji, ukubwa wa wastani wa uwekezaji katika kampuni zilizofungwa ni mdogo, hasa kwenye sekta ya utengenezaji, ambao ni dola za kimarekani milioni 4.2 tu, na haujafikia theluthi moja ya ukubwa wa wastani wa uwekezaji kwa kampuni mpya za utengenezaji ambao ni dola za kimarekani milioni 12.87. Bw. Tang Wenhong anasema,

    "Kwa kweli kampuni nyingi zilizofungwa ni kampuni hewa, moja kati ya tano ya kampuni zilizofungwa mwaka 2013 na mwaka 2014 hazikuzidi miaka mitatu, na kati ya kampuni hizo zilizofungwa, kamupuni zisizotiliwa mitaji zimefikia asilimia 60.3 na asilimia 63.2."

    Katika mji wa Dongguan ambao unaitwa "kiwanda cha dunia", mwaka jana pekee jumla ya viwanda 428 vya nchi za nje vilifungwa, vikiwemo viwanda maarufu kama Nokia na Liansheng Technology, na thamani ya uwekezaji ilifikia dola za kimarekani milioni 650. Hivi sasa kuna kampuni zaidi ya elfu 10 zilizowekezwa na wawekezaji wa nje, idadi ya kampuni zilizofungwa mwaka jana ni sawa na idadi hiyo mwaka 2013. Kutokana na kuongezeka kwa gharama ya nguvukazi, kati ya kampuni za nje zilizofungwa mwaka jana, idadi ya kampuni zilizoshughulikia utengenezaji wa jadi na kutumia nguvukazi nyingi imefikia 287, na kuchukua asilimia 70 kati yao. Katibu mkuu wa kamati ya wataalam ya Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Zhang Yansheng anaona kuwa, kampuni zinazotengeneza bidhaa zenye nyongeza ndogo ya thamani na kampuni zenye uwekezaji mdogo zimeondoka kutoka nchini China hatua kwa hatua, na hayo ni matokeo ya lazima yanayotokana na marekebisho ya muundo wa uchumi yanayoendelea nchini China. Anasema,

    "Kwa kampuni za nje zinazozingatia sana gharama za utengenezaji, zitahamisha viwanda vyao hadi nchi jirani kutoka sehemu ya delta ya mto Zhujiang."

    Wakati huo huo, mwaka jana, kampuni 465 zenye uwekezaji wa nje zimeanzishwa, na thamani ya uwekezaji huo imefikia dola za kimarekani bilioni 4.3, na thamani ya uwekezaji mpya kutoka nje imefikia dola za kimarekani bilioni 3.65. Mbali na hayo, mwaka 2014 idadi ya miradi ya huduma iliyowekezwa na wafanyabiashara wa nje imefikia 260 kutoka 110 ya mwaka 2008, hii ni mara ya kwanza kwa idadi ya miradi ya huduma kuzidi idadi ya miradi ya utengenezaji. Naibu mkurugenzi wa idara ya biashara ya kimataifa katika wizara ya biashara ya China Bi. Xing Houyuan amesema,

    "Kutumia uwekezaji wa nje kwa kiwango cha juu ni kauli mbiu ya sera kuhusu uwekezaji wa nje kwa sasa na katika muda ujao."

    Kuanzia mwezi Januari hadi Mei mwaka huu, uwekezaji wa nje nchini China umeongezeka. Katika kipindi hicho, idadi ya kampuni mpya zilizoanzishwa na wawekezaji wa nje nchini China imefikia 9,582, thamani ya zabuni imefikia yuan bilioni 771.55, na thamani ya matumizi halisi ya uwekezaji wa nje imefikia yuan bilioni 330.95, ambapo takwimu hizo tatu zimeongezeka kwa asilimia 9.6, 40.8 na 10.5. Mkurugenzi wa idara ya biashara ya nje katika wizara ya biashara ya China Bw. Tang Wenhong amesema,

    "Kwa jumla uwekezaji kutoka nje umeongezeka kwa utulivu, na muundo wa uwekezaji umeendelea kuboreshwa. Uwekezaji kwenye sekta ya utengenezaji wa hali ya juu umeongezeka kwa utulivu. Kuanzia mwezi Januari hadi Mei, uwekezaji wa nje kwenye sekta hiyo umeongezeka kwa asilimia 5.8. Hasa kwenye sekta za kemia, dawa, na utengenezaji wa vifaa vya elektroniki, matumizi ya mitaji ya nje yameongezeka kwa kiasi kikubwa zaidi."

    Kati ya sekta za utengenezaji zilizowekezwa na wafanyabiashara wa nje, sekta zinazotumia nguvukazi nyingi zikiwemo utengenezaji wa nguo na vifaa vya michezo ya watoto zimepungua, na sekta za utengenezaji zinazotumia teknolojia ya juu na bidhaa zenye nyongeza kubwa ya thamani zimeongezeka. Kwa mfano, sekta ya zana za mawasiliano na kompyuta zimechukua theluthi moja ya thamani ya matumzi halisi ya uwekezaji wa nje. Mwakilishi mkuu wa Benki ya Japan mjini Beijing Bw. Tomoyuki Fukumoto amesema,

    "Asilimia 47 ya kampuni zilizowekwa na wafanyabiashara wa Japan zinapanga kupanua biashara zao nchini China, hii inaonesha kuwa zina imani kuhusu mahitaji nchini China na soko la China. Vilevile China imekuwa na mlonlongo mkamilifu wa utoaji."

    Hivi sasa China inaongeza kasi ya kurekebisha muundo wa uchumi. Kuanzia mwaka 2013 sekta ya huduma imeanza kuchukua asilimia kubwa zaidi ya pato la taifa GDP kuliko sekta ya viwanda. Hadi kufikia robo ya kwanza ya mwaka huu, sekta ya huduma imechukua asilimia 51.6 ya GDP ya China. Wawekezaji wa nje wamegundua fursa ya maendeleo kwenye sekta ya huduma nchini China inayoendelezwa kwa kasi. Huko Xiaoshan mkoani Zhejiang, nyumba ya kutunza wazee inayojengwa imewekezwa dola za kimarekani milioni 30 na kampuni ya kutunza wazee ya Ufaransa na kampuni moja ya China. Baada ya kujengeka itakuwa nyumba ya kwanza ya kutunza wazee yenye ubia na nje mkoani Zhejiang. Bw. Tang Wenhong amesema,

    "China inazingatia kuondoa vizuizi kwa wawekezaji wa nje kuwekeza katika sekta za kuwatunza watoto na wazee, usanifu wa majengo, uhasibu, usambazaji bidhaa na biashara kwenye mtandao wa Interent."

    Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2014 thamani ya uwekezaji wa nje uliotumika kihalisi kwenye sekta ya huduma nchini China imefikia dola za kimarekani bilioni 6.63, ambayo ni ongezeko la asilimia 7.8 kuliko mwaka 2013, na kuchukua aslimia 55.4 ya uwekezaji wa jumla kutoka nje nchini China kwa mwaka huo. Katika miezi mitano ya mwanzo ya mwaka huu, kiwango hicho kimeendelea kuongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako