• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kusimamia ubora wa vyakula vya woto wachanga na wenye umri wa chini ya miaka mitatu

    (GMT+08:00) 2015-08-17 08:56:06

    Katika kipindi cha leo tutazungumzia kwa kina kuhusu usalama wa vyakula vya watoto, na tumeamua kuzungumzia hili kwa sababu katika miaka ya hivi karibuni, bidhaa zenye maandiko ya "chakula cha watoto" kama vile biskuti za watoto, soy sauce ya watoto, tambi za watoto na nyingine nyingi zinaonekana hapa na pale, na kupokewa vema na watoto na wazazi wao. Lakini swali ni je? Vyakula hivyo ni salama kwa kiasi gani kwa watoto? Wataalam wamedokeza kuwa, hivi sasa China bado haina kigezo maalum kinachohusu vyakula vya watoto, hivyo watu wanapozingatia lishe bora, pia wanapaswa kula kwa kiasi.

    Maana hata kama chakula unachokula kina lishe ya kutosha, unapozidisha kiasi unaweza kupata matatizo kadhaa kama vile kuvimbewa na kukosa raha. Sasa katika miaka ya hivi karibuni, vyakula vingi vinavyolenga watoto vimeibuka katika soko la China, kama vile soy sauce ya watoto, mafuta ya karanga, tambi za watoto, na vingine vingi, na bei za bidhaa hizo ni kubwa, lakini zinapendwa na wazazi kutokana na kudai kuwa zina chumvi kidogo na lishe bora.

    "Sosi ya soy ambayo ni organic tunayonunua ni maalum kwa ajili ya watoto, ina madini ya chuma, zinki, na calcium, aidha imeandikwa kuwa haikuongezwa kitu chochote na dawa za kuhifadhi ili isiharibike, hivyo ingawa bei yake ni kubwa, lakini tuna mtoto mmoja tu, basi."

    "Nilinunua biskuti ya watoto na cereal."

    "Niliwahi kununua tambi za watoto na haradali za watoto."

    "Nilinunua sosi ya soy ya watoto, na mafuta ya karanga ya watoto. Bei ya mafuta hayo ni Yuan 100, chupa ndogo, na chupa ndogo ya sosi ya soya ya watoto ni Yuan 70. Lakini tuna mtoto mmoja tu, tunampenda."

    Ndivyo wanavyosema wazazi hao ambao wanafurahia vyakula hivyo. Lakini vyakula hivyo kweli ni salama? Hivi karibuni, kitengo cha utafiti wa lishe na usalama wa chakula kilicho chini ya Chuo cha utafiti wa dawa za kinga cha China ilifanya ukaguzi wa vyakula 114 vya watoto vyenye lishe. Matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa, theluthi moja ya vyakula hivyo havina virutubisho, theluthi nyingine moja ya vyakula vina virutubisho lakini hazijafikia kigezo kama ilivyoandikwa. Mtafiti wa kituo cha tathimini ya hatari ya usalama wa chakula Han Junhua amesema, nchini China licha ya vyakula vya lazima kwa watoto wachanga wenye umri wa miaka chini ya mitatu, hivi sasa hakuna kigezo husika kuhusu "vyakula vya watoto". Vyakula vinavyoandikwa "vya watoto" sokoni ni propaganda ya wafanyabiashara tu, ubora wa bidhaa hizo unaweza kusimamiwa kwa kufuata kigezo cha vyakula vya kawaida, kama vinafaa watoto kula au la vinaamuliwa na dhamira ya wafanyabiashara. Han amesema,

    "Nchini China tuna vigezo vya vyakula vinavyolenga watoto wachanga wenye umri wa miaka chini ya mitatu, kama vile, chakula cha watoto wachanga, chakula cha watoto wachanga na wadogo, virutubisho vya nafaka kwa watoto hao, vyakula vya makopo vya watoto hao, na vyakula maalum vya kitabibu kwa watoto wachanga. Vigezo hivyo vinaweza kuhakikisha usalama wa watoto wenye umri wa miaka chini ya mitatu."

    Vyakula vimeandikwa ni vya watoto lakini hakuna kigezo cha kupima kama kweli vinafaa kwa watoto. Han Junhua amesema, baada ya kuwasiliana na chanzo kimoja amegundua kuwa, hivi sasa nchi zote duniani hazina vigezo vinavyolenga vyakula vya watoto, lakini nchi zilizoendelea zinawalinda watoto kupitia maelezo yaliyowekwa kwenye vyakula hivyo, maelezo yaliyopo kwenye matangazo, n.k. na kwamba ni vizuri kujifunza kutoka kwao. Han amesema,

    "Kwa watoto wenye umri wa zaidi ya miaka mitatu, baadhi ya nchi zilizoendelea zinawalinda kupitia matangazo, maelezo yaliyowekwa kwenye bidhaa husika, au vikwazo kwa maeneo karibu na shule. Kwa mfano, sheria ya Marekani inasema kuwa haiwezi kutoa matangazo kwa vyakula vyenye sukari nyingi na chumvi nyingi; na katika maeneo ndani ya mita kadhaa ya shule, hairuhusiwi kuuza vyakula vidogovidogo"

    Hivi karibuni suala la usalama wa vyakula linalotokea katika maeneo karibu na shule yanayouza vitafunwa pia linafuatiliwa sana na jamii ya China. "Vitafunwa vya senti 50" ambavyo vinatengenezwa kiholela vinauzwa karibu na shule, na kutokana na rangi zao za kupendeza na ladha nzuri, zinapendwa na watoto. Lakini vitafunwa hivyo vina viungo vingi sana, ambavyo vikilinbikizwa mwilini vinaweza kusababisha vidonda.

    Hiyo kweli ni hatari hususan kwa watoto wadogo. Sasa ili kukabiliana na suala hilo la kuwa na viungo vingi, sukari nyingi, chumvi nyingi na mafuta mengi katika vyakula vya watoto, Han Junhua amesema, kigezo kipya cha chakula kilichoanza kutekelezwa mwezi Mei mwaka huu, kimefanya marekebisho mengi juu ya vyakula vya watoto. Anasema,

    "Katika marekebisho ya vigezo vya chakula (GB2760-2011), matumizi ya viungo vinavyoongezwa kwenye vyakula chenye Aluminum yamepigwa marufuku. Kwa kuwa vyakula hivyo vinaliwa zaidi na watoto, hivyo hatua hii inaweza kuwalinda watoto wasile sana aluminum."

    Han Junhua amesisitiza kuwa, ili kuhakikisha usalama wa vyakula kwa watoto, ni muhimu kuzingatia matumizi ya chakula kiafya. Kwa mfano idara ya afya ya China iliwahi kutoa Mwongozo wa matumizi ya vitafunwa kwa watoto na vijana wa China, ambao unagawa vitafunwa hivyo katika ngazi tatu. Kuna zinazoweza kuliwa mara kwa mara, zinazoliwa kwa wakati maalum, na zenye ukomo wa kula, hivyo wazazi wanaweza kununua vitafunwa kwa kufuata mwongozo huo, na kutoa maelekezo husika kwa watoto wao. Aidha, idara za usimamizi pia zinapaswa kusimamia mazingira karibu na shule, na kuzuia vyakula visivyo na ubora kuingia sokoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako