• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yathibitisha kutoa msamaha kwa wafungwa katika maadhimisho ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia

    (GMT+08:00) 2015-08-30 18:54:00

    Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kimepitisha mpango wa kutoa msamaha kwa wafungwa ambapo maelfu ya maveterani wa vita dhidi ya uvamizi wa Japan na wafungwa ambao ni wazee sana, vijana, au wagonjwa wataachiliwa kwa msamaha, ikiwa ni moja ya shuhguli za maadhimisho ya miaka 70 ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia hapo Septemba 3.

    Mpango huo uliotangazwa rasmi na rais Xi Jinping wa China hapo jana, unafanyika miaka 40 baada ya China kutoa msamaha kwa wafungwa wa kivita mwaka 1975, na miaka 56 baada ya msamaha wa kwanza kutolewa kwa wafungwa wasio wa kivita mwaka 1959. Msamaha huu ni wa nane kutolewa tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

    Aina 4 za wafungwa wataweza kupata msamaha huu, wakiwemo wahalifu waliopigana vita dhidi ya uvamizi wa Japan na vita ya ukombozi, wahalifu walioshiriki kwenye vita ya kulinda mamkala ya nchi, usalama, na ukamilifu wa ardhi ya nchi baada ya mwaka 1949, isipokuwa wale waliokutwa na makosa ya uhalifu mkubwa kama matumizi mabaya ya fedha, rushwa, ugaidi, na kupanga uhalifu. Pia wafungwa wenye umri wa zaidi ya miaka 75, na wale wenye ulemavu unaowafanya washindwe kujihudumia, na aina ya mwisho ya wafungwa wanaoweza kupata msamaha ni wale waliofanya uhalifu wakiwa na umri wa chini ya miaka 18 na kupata hukumu ya hadi miaka mitatu jela.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako