• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi wa bunge Misri kufanyika kuanzia tarehe18 mwezi Oktoba

    (GMT+08:00) 2015-08-31 10:17:45

    Tume ya uchaguzi ya Misri jana huko Cairo imetangaza kuwa uchaguzi wa bunge la awamu mpya utafanyika kuanzia tarehe 18, Oktoba.

    Mkurugenzi wa tume hiyo Bw. Ayman Abbas amesema, uchaguzi huo utafanyika kwa vipindi viwili katika mikoa 27. Katika kipindi cha kwanza, uchaguzi utafanyika tarehe 18 na 19 Oktoba katika mikoa 14 ikiwemo Giza, Alexandaria na Faiyum. Na uchaguzi katika mikoa 13 mingine utafanyika tarehe 23 na 24 mwezi Novemba.

    Mwezi Januari mwaka huu, tume ya uchaguzi ya Misri ilitangaza kuwa uchaguzi wa bunge utafanyika kuanzia mwezi Machi, lakini mahakama ya katiba ya Misri ilisema sheria kuhusu majimbo ya uchaguzi wa bunge inakiuka katiba ya nchi hiyo, hivyo rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri aliamuru kutunga upya sheria hiyo, na kuahirisha uchaguzi wa bunge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako