• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatawala michuano ya riadha ya dunia jijini Beijing

    (GMT+08:00) 2015-08-31 15:01:25
    Kenya imeandika historia ya kuwa nchi bora kwa upande wa mbio na michezo ya uwanjani baada ya kuongoza katika michuano ya riadha ya Dunia iliyomalizika katika uwanja wa Bird's Nest mjini Beijing siku ya jumapili.

    Kenya imedhihirisha kuwa ni taifa bora katika riadha baada ya kunyakua idadi ya medali 16 , saba zikiwa za dhahabu, sita za fedha na tatu za shaba.

    Jamaica imeshika nafasi ya pili kwa idadi ya medali 12, saba za dhahabu, mbili za fedha na tatu za shaba huku Marekani imemaliza nafasi ya tatu ikiwa na jumla medali 18 zikiwemo dhahabu sita, fedha sita na shaba sita.

    Mashabiki nchini Kenya wameipongeza timu yao ambayo imevuka asili yake ya kutawala katika mbio za kati na ndefu kufuatia pia kufanya vema katika mbio fupi na michezo mingine uwanjani.

    Raia Uhuru Kenyatta alikuwa wa kwanza kuwapongeza wanariadha wa Kenya kwa kiwango bora walichokionesha.

    Rais Kenyata amesema wanamichezo hao wameionesha dunia kuwa wana vipaji, nidhamu, malengo, ushirkiano wa timu na maono ya kufanya vema katika kiwango cha juu.

    Katika mashindano matatu yaliyopita, Kenya imemaliza katika nafasi tano za juu.

    Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya olimpiki ya Kenya (NOCK) Kipchoge Keino anasema Kenya imekuwa na hisia nzuri jijini Beijing.

    Mwaka 1996 David Rudisha aliiongoza Kenya kushinda michuano ya vijana ya dunia jijini Beijing. Miaka 12 baadaye Kenya ilifanya vema katika michuano ya Olimpiki mwaka 2008 jijini Beijing na mwaka huu 2015 jijini Beijing Kenya imekuwa mshindi wa jumla.

    Ushindi wa mbio fupi za mita 400 kuruka vihunzi kwa Nicklas Bett na ushindi wa kurusha mkuki kwa Julius Yego umebadilisha mlingano juu ya Kenya.

    Makamu wa rais wa chama cha riadha cha Kenya David Okeyo amesema wataimarisha ustadi huo mzuri kuelekea michuano ya Olimpiki ya mwaka 2016 mjini Rio De Janeiro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako