• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 70 na askari 8 wauawa katika mapigano nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2015-08-31 17:46:43

    Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imesema, wapiganaji 70 wa kundi la Taliban na askari 8 wa jeshi la nchi hiyo wameuawa wakati wa operesheni ya kijeshi na mapigano yaliyotokea ndani ya saa 24 nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema, wapiganaji wengine 45 wamejeruhiwa na gaidi mmoja amekamatwa katika operesheni hiyo iliyofanyika katika maeneo mbalimbali nchini Afghanistan.

    Wataalam wa jeshi waligundua na kutegua mabomu kadhaa yaliyofukiwa chini ya ardhi na yaliyotegwa kando ya barabara, pia jeshi hilo limekamata kiasi kikubwa cha risasi na silaha.

    Kundi la Taliban halijatoa kauli yoyote kuhusuana na tukio hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako