• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanamke anawezaje kutoa uwiano sawa kwa kazi yake na familia?

    (GMT+08:00) 2015-09-07 14:51:49

    Mfumo dume kwa kiasi fulani bado unatawala katika nchi mbalimbali, hususan zile zinazoendelea, ambapo mwanamke anachukuliwa kama chombo cha starehe, na kazi yake kubwa ni kumhudumia mumewe, watoto, na kusimamia nyumba. Mwenzangu Caroline Nassoro alifanya mahojiano na Jane Munji Maina, meneja wa matangazo ya biashara kwenye kituo cha televisheni cha KTN na Radio Maisha vinavyomilikiwa na kampuni ya Standard Group ya Kenya. Na anaanza kwa kueleza changamoto alizokutana nazo hadi kufikia nafasi aliyo nayo sasa, na jinsi gani anaweza kuwa na uwiano kati ya familia, masomo, na kazi.

    Jane Munji akieleza changamoto na jinsi anavyoweza kuleta uwiano katika mambo muhimu kwake, familia, masomo, na kazi. Kutokana na maelezo yake, sote tunakubali kuwa kila kitu ni kujipanga, ukiwa na mpangilio mzuri, utafanikisha kila unalopanga kulifanya. Lakini, msaada wa watu wengine, hususan ndugu, nao unahitajika ili kuweza kutimiza hilo. Barani Afrika familia ni kubwa, ndugu ni wengi, ambao wako tayari kutoa msaada pale unapohitajika, kwa kadri ya uwezo wao. Jane naye anasema, ndugu pia wamekuwa msaada mkubwa sana kwake katika kutimiza majukumu yake, na ana ushauri gani kwa wanawake wengine barani Afrika?

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako