• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la zamani la kutengeneza kauri la Tongguan Yao mjini Changsha, Hunan

    (GMT+08:00) 2015-09-16 10:09:21

    Changsha ni mji maarufu ulioko moani Hunan, wa kihistoria, una utajiri mkubwa wa mandhari ya kuvutia na ni chimbuko la watu wengi maarufu nchini China. Kadri miji inavyopanuka na shughuli za kibinadamu kuendelea, miji mingi aidha imehamishwa au kubadilishwa majina, lakini kwa mji wa Changsha, jina na sehemu ulipo havijabadilishwa kwa miaka 3000 iliyopia. Mji huu uliwahi kufahamika kama makazi ya mshairi maarufu Qu Yuan na mwanasiasa maarufu ambaye pia ni mwanzilishi wa taifa la China Mao Tse Tong. Baraza la serikali la China limeuorodhesha mji huu miongoni mwa miji marufu 24 ya kihistoria na kitamaduni.

    Kwa upande wa utamaduni, mji wa Changsha una vivutio kemkem vya utamaduni, likiwepo eneo la kutengeneza kauri la Tongguan Yao. Kijiografia, eneo hili liko katika wilaya ya Tongguan, mji wa Wangcheng, mjini Changsha, sio mbali na mto Xiang.

    Katika eneo hili, kuna mabaki ya vyombo vya kauri vilivyotengenezwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita, enzi za mfalme Tang. Kutokana na historia ya eneo hilo, inaaminika kuwa wafanyabiashara kutoka nchi za Uarabuni walikuwa ni wanunuzi wa vyombo vya kauri vilivyotengenezwa hapo, na hata waliweza kuleta oda maalum na kutengenezewa. Wateja wa vyombo hivyo walitoka sehemu malimbali duniani, ikiwemo Afrika kaskazini na mashariki.

    Hivi sasa sehemu hiyo imekuwa kama jumba la makumbusho ya utengenezaji wa kauri. Lakini umbali mchache kutoka kwenye eneo hilo, kilomita kama 5 hivi, kuna mtaa wa kale, ambako pia wakazi wake wanaendeleza utamaduni wa kutengeneza kauri na kuziuza kwa wafanyabiasha kutoka sehemu mbalimbali hapa China. Katika mtaa huo wa kale unaoitwa Tongguan ambao pia ni kivutio cha utalii, bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kwa kauri zinauzwa kwa jumla na hata rejareja kwa watalii, kuna migahawa inayouza chakula cha asili cha mahali hapa, na pia kuna migahawa ambamo watu, hususan wa makamo, hukutana na kucheza mchezo wa Mahjong ambao ni maarufu sana hapa China.

    Ukipata fursa ya kutembelea mji wa Changsha, usikose kutembelea eneo hilo la Tongguan Yao pamoja na mtaa huo wa Tongguan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako