• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanawake wa mashinani Kenya wapiga hatua kiuchumi kupitia mikopo ya serikali

    (GMT+08:00) 2015-10-16 09:16:49

    Tarehe 15 Oktoba ikiwa ni siku ya Umoja wa Mataifa ya wanawake wanaoishi mashambani, nimefika hapa kaunti ya Kakamega magharibi mwa Keny ambapo nimekutana na vikundi tofauti vya wanawake, ambavyo vimesaidiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali, serikali kuu na serikali ya kaunti hili kuanzisha miradi ya kujikimu kimaisha.

    Katika sehemu ya pili ya makala yetu nimetembelea eneo ambalo kina mama hawa wa kikundi kiitwacho Krusi wanafanya mradi wa ufugaji kuku.

    Hapa nakutana na Bi. Florence ambaye hii leo ni zamu yake ya kuwapatia kuku hao chakula. Bi. Florence ananieleza baadhi ya changamoto wanazo pitia katika mradi huu wa kuku.

    Kwanza anasema kupata soko ni ngumu sana, kwani ni vigumu sana kupata mahali pamoja pakupeleka kuku, pia anasema wanapata changamoto ya kutafuta soko.

    Hata hivyo Bi.Barasa ambaye ni moja wa wanawake wa kikundi hiki anasema kando na kukosa soko pia upata changamoto ya kudharauliwa katika mambo ya kimaendeleo na kibiashara.

    Lakini kina mama hawa matarajio na matumaini yao ni kupata soko la pamoja kuweza kuuza vitu zao kwa pamoja na kupata mapato mazuri.

    Bi. Chitsia anasema wana furahia jinsi mashirika tofauti yana wasaidia kifedha, lakini wanataka mabadiliko ya mikopo kuwa mikubwa kidogo kwa maana ile wanayo pewa hivi sasa ni kidogo.

    Kina mama hawa wanatambua juhudi za mashirika yanayo wasaidia fedha ama kwa njia ile yoyote.

    Hivi sasa kina mama mashinani wamefunguka macho na kuweza kupingania haki zao na pia kuania vyeo vikubwa serikali bila uonga.

    Pia serikali kuu inatumia njia kadhaa kuwainua wa mama mashinani, kama vile kuwapa elimu ya bure ya maendeleo, kuwapa nafasi kuingilia miradi ya ufumbuzi na pia kuwapa fursa katika uongozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako