• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF ina uhakika na uchumi wa China

    (GMT+08:00) 2015-10-09 16:07:49

    Naibu mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Zhu Min amesema, mageuzi ya mfumo na uzalishaji wa nguvu kazi ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa China.

    Zhu amesema hayo jana, kabla ya mkutano wa mwaka wa Kundi la Benki ya Dunia unaofanyika kuanzia leo huko Lima, Peru.

    Hivi karibuni, IMF ilipunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka huu kuwa ni asilimia 3.1, ikiwa ni chini zaidi ya makadirio ya awali ya asilimia 3.3. Hata hivyo, makadirio yake kwa ongezeko la pato la taifa la China GDP imeendelea kubaki asilimia 6.8 kwa mwaka huu. Amesema ukuaji wa polepole wa uchumi wa China hauwezi kulazimishwa kuongeza kasi kwa kuwa unapunguza hatari na wakati huohuo, kuimarisha ubora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako