• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yapongeza mashambulizi ya anga yanayofanywa na Russia dhidi ya magaidi nchini Syria

    (GMT+08:00) 2015-10-09 17:50:47

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran kuhusu masuala ya Uarabuni na Afrika Hossein Amir-Abdollahian amesema, nchi yake inapongeza mashambulizi ya anga yanayofanywa na Russia na operesheni za kijeshi nchini Syria dhidi ya makundi ya kigaidi.

    Naibu waziri huyo amesema, hatua hiyo ya Russia ni muhimu na mwafaka katika mapambano dhidi ya ugaidi katika kanda hiyo, kutokana na kutofanikiwa kwa operesheni inayoongozwa na Marekani dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Syria zilizoanza mwaka jana.

    Ameongeza kuwa, Iran itaendelea kuziunga mkono serikali za Syria na Iraq katika mapambano yao dhidi ya ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako