• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yakamilisha mipango ya kununua umeme Kenya.

    (GMT+08:00) 2015-10-09 19:56:22

    Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa tayari imekamilisha mipango ya kununua kawi kutoka nchini Kenya.

    Kulingana na khabari kutoka kwa gazeti moja la kila siku nchini humo ni kwamba nchi hiyo sasa itakuwa ikiagiza mega wati 30 za umeme kutoka nchini Kenya.

    Afisa mkuu wa kampuni ya kawi nchini Rwanda ya Rwanda Energy Jean Bosco Muginarenza, anasema anasema tayari dola milioni 50 walizopata kutoka kwa benki ya maendeleo barani Afrika AfDB na shirika la msaada la Japan JICA ndizo zinatumika kufadhili mradi huo.

    Aidha serikali ya Kenya inasema mwaka jana ilitia saini makubaliano na serikali ya Rwanda kuanza mradi huo wa kuiuzia Rwanda kawi hiyo ya mega wati 30.

    Kwa sasa Rwanda ina uwezo wa kuzalisha mega wati 162. 2 lakini inataka kufikia mega wati 563 kabla ya mwaka wa 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako