Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China leo imekutana chini ya katibu wa Chama hicho Bw. Xi Jinping na kujadili masuala muhimu kuhusu mpango wa 13 wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya kipindi cha miaka mitano. Mkutano huo pia umepitisha kanuni za nidhamu za chama na adhabu kwa vitendo vya kukiuka kanuni hizo.
Mkutano huo umeamua kuwa mkutano wa 5 wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 18 ya chama cha kikomunisti cha China utafanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 mwezi huu hapa Beijing.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |