• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dar yataka kukata utegemeaji wa nishati ya maji

    (GMT+08:00) 2015-10-26 20:58:05
    Tanzania inatarajiwa kupunguza utegemezi wa umeme wa maji kwa asilimia 15 baada ya miradi ya nishati ya Kinyerezi II na Kilwa kuanza kazi kikamilifu.

    Hivi sasa, utegemezi wa umeme wa maji ni zaidi ya asilimia 60, hivyo kujenga uhaba mkubwa wa umeme hasa wakati wa kiangazi.

    Haya yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji BW: Felchesmi Mramba, wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO ), jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

    Bw Mramba anasema, utekelezaji wa mradi wa Kinyerezi II unatarajiwa kuanza mwezi ujao.

    Mradi wa Kinyerezi II itatengenezwa na shirika la Japan Sumitomo na itakuwa na uwezo wa Megawati 240.

    Fedha za kufadhili mradi huu nikutoka kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Japan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako