• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote wawa matarajio mapya wa wananchi wa China

    (GMT+08:00) 2015-11-02 15:57:22

    Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China umepitisha pendekezo la kutunga mpango kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii katika miaka tano ijayo, na kutoa malengo mapya kuhusu kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, ambayo yametoa matarajio mapya ya Wachina.

    Taarifa iliyotolewa na mkutano huo imesisitiza kuwa miaka mitano ijayo ni kipindi muhimu katika ujenzi wa jamii yenye maisha bora, na mpango kuhusu miaka mitano ijayo unatakiwa kutungwa kwa ajili ya kufanikisha lengo hilo. Wakizungumzia jinsi wanavyoelewa jamii yenye maisha bora, watu wa kawaida nchini China wanasema,

    "Watu wanaona furaha kuwa na maisha mazuri, na siasa iwe safi. Kama malengo hayo mawili yakitimizwa, jamii yenye maisha bora inapatikana."

    "Naona katika jamii yenye maisha bora, kuna haki, siasa ni safi na maisha ya watu ni mazuri, watu wanaishi kwa masikilizano na kukubali mambo tofauti."

    "Watu wanaona utulivu na furaha katika jamii yenye maisha bora, na hawana haja ya kuwa na wasiwasi na siku zao za baadaye."

    Je, jamii yenye maisha bora ni jamii ya aina gani? Naibu mkurugenzi wa kikundi kinachoshughulikia mambo ya fedha cha Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Yang Weimin anasema,

    "Jamii yenye maisha bora si lengo linalohusu tu maendeleo ya uchumi na maisha ya watu, bali ni jamii ambako uchumi unaendelezwa, demokrasia na utawala wa sheria vinakamilika, utamaduni unang'ara, watu wanaishi kwa masikilizano, maisha ya watu yanazidi kuwa mazuri, na pia mazingira yameboreshwa na sera zinakamilika."

    Katika jamii yenye maisha bora kwa pande zote, watu wanaishi maisha mazuri, lakini maendeleo ni sharti la kwanza, msingi na jambo muhimu. Katika miaka mitano ijayo, uchumi wa China utaendelea kukua kwa kasi ya kiasi hadi kubwa. Hivi sasa, uchumi wa China umeingia katika hali mpya ya kawaida, na kasi ya ukuaji na ubora wa uchumi vinafuatiliwa nchini na nje ya nchi. Naibu mkuu wa kitivo cha utawala na mambo ya fedha cha Chuo Kikuu cha umma cha China Zhao Xijun anasema lengo la kujenga jamii yenye maisha bora litatimizwa kama uchumi wa China unaweza kukua kwa kiwango kilichowekwa, kwa hiyo kuna changamoto kubwa katika kufanikisha lengo hilo.

    "Ujenzi wa jamii yenye maisha bora utafanikishwa kama pato la taifa la China kwa mtu mmoja mmoja litaongezeka kwa mara mbili. Tunaweza kutimiza lengo hilo, lakini bado tunakabiliwa na changamoto kubwa kiasi. Kwanza, jinsi ya kuboresha sekta za kiviwanda tulizo nazo sasa, na kubadilisha njia za uzalishaji viwandani za sasa jadi kuwa za kisasa. Pili ni jinsi ya kuendeleza vizuri maeneo yaliyoibuka hivi karibuni ya kimkakati, na kuweka nguvu mpya kwa maendeleo ya uchumi katika siku zijazo."

    Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China umeagiza kuwa uchumi utakua kwa kasi ya kiasi na hadi kubwa, na pia umesisitiza kuwa maendeleo ya uchumi yatakuwa ya uwiano, jumuishi na endelevu. Wataalamu wanasema China itatilia maanani zaidi ubora wa ongezeko la uchumi na jinsi ya kushughulikia suala la kuishi kwa masikilizano kati ya uchumi, mazingira na jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako