Viwanda vya uvumbuzi na teknolojia ya juu vimeibuka kuwa nguvu mpya ya kuchochea ukuaji wa uchumi wa China.
Hayo yamesemwa na Zhang Yongwei, naibu mkurugenzi mkuu wa kituo cha utafiti wa viwanda, kilicho chini ya Kituo cha Utafiti wa Maendeleo cha Baraza la Serikali la China. Amesema ukuaji katika sekta ya teknolojia utasaidia kuinua viwanda vya asili vinavyokufa kama uchomaji wa chuma. Amesema maeneo ya maendeleo ya teknolojia ya juu na uvumbuzi yanaongezeka na kuwa nguvu muhimu ya maendeleo ya kikanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |