• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pato la mtu mmoja mmoja nchini China lafikia dola za kimarekani 7,800

    (GMT+08:00) 2015-11-03 16:18:09

    Pato la mtu mmoja mmoja nchini China limeongezeka na kufikia dola za kimarekani 7,800.

    Hayo yamo kwenye waraka rasmi uliotolewa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC kuhusu Mapendekezo ya Kutunga Mpango wa miaka mitano ijayo wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii, ambao ulipitishwa katika kikao cha 5 cha kamati kuu ya 18 ya CPC kilichomalizika mwisho wa mwezi uliopita.

    Waraka huo pia umesema CPC imerejea tena dhamira yake ya kupambana na umasikini, na kuahidi kuongeza msaada wa kifedha kwa maeneo masikini zaidi katika mpango huo wa miaka mitano. Hayo yatatimia kwa kupunguza pengo la kipato na kuongeza idadi ya watu wenye kipato cha kati katika miaka mitano ijayo.

    Waraka huo pia umesema China itaendelea kufungua zaidi uchumi wake ili kuvutia uwekezaji wa kigeni na kuzishawishi kampuni za China kuwekeza nchi za nje. China pia itaanzisha Mfuko wa Maendeleo wa Kijani, ili kuimarisha uzalishaji usiochafua mazingira na ukuaji endelevu.

    Katika miaka mitano ijayo, China itaongeza ushindani wa kibiashara kwa kufungua sekta za mafuta, gesi asilia, umeme, mawasiliano ya simu, usafiri, na miundombinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako