• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya ndani ya China yaonesha kuwa na imani ya muskabali mzuri katika soko la China

    (GMT+08:00) 2015-11-03 16:50:25

    Tovuti ya uchumi ya China hivi karibuni ilichapisha makala iliyotolewa na naibu mkurugenzi wa idara ya utafiti wa kampuni ya Kituo cha Utafiti wa Maendeleo cha Baraza la Serikali la China Zhang Yongwei, akielezea kuhusu imani ya makampuni ya China kuhusu mwelekeo wa hali ya soko la China katika mazingira mapya kiuchumi.

    Ripoti iliyotolewa na Shirika la Habari za Kimataifa kuhusu Soko MIN lililo chini ya Kampuni ya Soko la Hisa ya Ujerumani DBAG, inasema imani ya makampuni ya China iliongezeka kwa asilimia 8.3 katika mwezi Oktoba kuliko mwezi Septemba, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi tangu mwezi Machi mwaka 2011. Hii ni ishara muhimu inayoonyesha kuwa makampuni ya China yamefanya jitihada katika kuchukua hatua za kukabiliana na shinikizo linalotokana na kupungua kwa kasi ya ongezeko la uchumi na kurekebisha shughuli zao za kibiashara, na kwamba yana imani kubwa na uchumi wa China katika siku za baadaye. Makampuni mengi yaliyoanza mapema mageuzi na yenye uwezo mkubwa wa teknolojia yamekuwa nguvu muhimu katika kuendeleza uchumi.

    Kuanzia mwezi Januari hadi Julai, uwekezaji uliofanywa katika mageuzi ya teknolojia za kiviwanda ulifikia Yuan trilioni 4.3376, kiasi ambacho ni ongezeko la asilimia 12.9 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Uwekezaji katika teknolojia ni uwekezaji kwa ajili ya siku za baadaye, na ongezeko la uwekezaji katika mageuzi ya teknolojia ni ushahidi mkubwa unaoonesha imani ya makampuni. Makampuni mengi yameanza kutambua kuwa njia muhimu ya kujikwamua kutoka hali ya bidhaa kuzalishwa kwa wingi kupita kiasi na ushindani mbaya wa bei nafuu ni kutegemea uvumbuzi na kuongeza ufanisi na teknolojia.

    Sekta mpya zilizoibuka hivi karibuni zinaendelezwa kwa kasi, na kuziba pengo la ongezeko linalotokana na kuzorota kwa sekta za jadi. Mikoa iliyopo mashariki mwa China yenye mazingira mazuri kwa uvumbuzi na masoko mazuri imeweka nguvu mpya kwa ongezeko la uchumi, na maeneo ya uendelezaji wa teknolojia ya juu yanayosisitiza uvumbuzi pia yamekuwa injini muhimu ya ukuaji wa uchumi. Sekta zilizop nyuma kimaendeleo zinajitoa kwenye soko, na sekta za teknolojia ya hali ya juu na sekta zilizoibuka hivi karibuni zinachangia zaidi ukuaji wa uchumi. Ugatuzi umeongeza idadi ya makampuni mapya. Kuanzia mwezi Machi mwaka 2014 hadi mwezi Agosti mwaka jana, makampuni yaliyosajiriwa yamefikia milioni 20.814 kote nchini China, idadi ambayo ni ongezeko la asilimia 16.

    Kuna makampuni ya aina tatu yenye imani ni mustakabali wa uchumi wa China, yaani makampuni yanayoendeleza biashara zao hatua kwa hatua bila ya kuhangaika, makampuni yanayotilia maanani uvumbuzi na yale yaliyoanza mageuzi mapema. Pia hatua kabambe zilizotangazwa katika siku za hivi karibuni kuhusu kuhimiza maendeleo tulivu na mageuzi ya kimuundo zimeanza kuonesha ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako