• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mapendekezo ya mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano

    (GMT+08:00) 2015-11-04 10:55:38

    Chama cha Kikomunisti cha China CPC kimetoa mapendekezo kwa ajili ya maendeleo ya taifa ya miaka mitano ijayo.

    Mapendekezo hayo kuhusu mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano (2016-2020) ya uchumi na jamii yalikubaliwa kwenye Mkutano wa 5 wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 18 ya CPC uliofungwa mwishoni mwa mwezi uliopita.

    Katika mapendekezo hayo, kipindi cha miaka mitano ijayo kilielezwa kama ni kipindi muhimu katika kujenga kwa pande zote jamii yenye maisha bora ifikapo mwaka 2020, ambapo China inataka kufanya thamani ya jumla ya uzalishaji GDP na wastani wa pato la mtu mmoja mmoja viwe mara mbili ya ile ya mwaka 2010. Mapendekezo hayo yamesisitiza uvumbuzi, ushirikiano, maendeleo bila uchafuzi, ufunguaji mlango na kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako