• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo kuhusu kutunga mpango wa miaka mitano ijayo wa maendeleo ya China lajumuisha mambo makuu matatu

    (GMT+08:00) 2015-11-04 16:44:59

    Chama cha Kikomunisti cha China CPC kimetangaza pendekezo kuhusu kutunga Mpango wa Miaka Mitano Ijayo wa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii ya China, lililopitishwa katika kikao cha 5 cha wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 18 ya CPC kilichomalizika Oktoba, 29. Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Taifa ya China Xu Shaoshi anasema pendekezo hilo lina mambo makuu matatu, na China ina nia na uwezo wa kufanya uchumi wake uongezeke kwa kasi ya kati na hadi kubwa.

    Bw Xu amesema pendekezo hili linajumuisha mambo makuu matatu, ambayo ni pamoja na kuhimiza maendeleo ya aina 5 ya uvumbuzi, uratibu, ulinzi wa mazingira, ufunguaji na mabadiliano; kulinda hadhi kuu ya wananchi, maendeleo ya kisayansi, mageuzi kamili, utawala wa kisheria, uratibu wa masuala ya ndani na nje ya nchi na uongozi wa Chama. Pia lilitoa malengo mapya kwa kazi za kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

    "Pendekezo hilo linaweka malengo matano katika ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote, ambayo ni pamoja na uchumi kuongezeka kwa kasi ya kati na hadi kubwa, kiwango cha maisha ya watu kuongezeka, sifa ya wananchi na kiwango cha ustaarabu wa jamii kuongezeka kidhahiri, mazingira ya asili kuboreshwa na kukamilisha sera za aina mbalimbali."

    Lengo lililotolewa kwenye mpango wa miaka mitano ijayo kuhusu ukuaji wa uchumi pia linafuatiliwa sana. Bw Xu amesema pato la taifa la China na pato la wastani la mtu vitaongezeka na kuwa mara 2 kuliko mwaka 2010, lengo ambalo si rahisi kutimizwa kama uchumi usipokua kwa kasi fulani. Ameongeza kuwa kwa mujibu wa mazingira ya nchini na nje ya nchi, lengo la kufanya ukuaji wa uchumi uongezeke kwa kasi ya kati na kubwa linaweza kutimizwa.

    "Kimataifa, amani na maendeleo ni mwelekeo mkuu wa karne hii, huku China ikiwa katika kipindi cha fursa za kimkakati, inaweza kufanikisha mambo mengi. Sababu nyingine muhimu ni kuwa raundi ijayo ya ufufuaji na ukuaji wa uchumi vitaamuliwa na mageuzi ya teknolojia na kiviwanda, jambo ambalo linaendana na msisitizo wa China kujiendeleza kupitia uvumbuzi, hii imetoa fursa kwa China. Nchini China kuna fursa nyingi za maendeleo, mahitaji kwa soko yatatolewa katika mchakato wa ukuaji wa miji, na ufanisi wa maendeleo kupitia uvumbuzi unaongezeka. Pia kuna sababu nyingine muhimu. Tuna watu bilioni 1.3, nguvukazi milioni 900, na makampuni milioni 70, kwa hiyo uchumi unaweza kuendelezwa zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako