Naibu mkurugenzi wa Idara ya Kuzuia Rushwa ya China Liu Jianchao amesema China iko makini katika kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimataifa uliopo katika eneo la kuzuia rushwa, na kutoa wito kwa mikakati mipya ya kufuatilia bidhaa zilizopotea na kuwakamata watuhumiwa.
Liu, ambaye pia ni mkurugenzi wa idara ya ushirikiano wa kimataifa iliyo chini ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Ukaguzi wa Nidhamu, amesema hayo alipohudhuria kikao cha 6 cha Mkutano wa Nchi zilizosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Rushwa UNCAC. Amesema mapambano dhidi ya ufisadi ni changamoto kubwa inayoikabili jumuiya ya kimataifa, na ni muhimu katika juhudi zinazofanywa na Chama cha Kikomunisti cha China ili kutimiza haki ya jamii, kulinda mfumo wa sheria wa China, na kuboresha utawala wa sheria.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |