• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ongezeko la asilimia 6.5 ni matarajio ya msingi, na si lengo la uchumi wa China katika miaka 5 ijayo

    (GMT+08:00) 2015-11-09 18:45:29

    Naibu mkurugenzi wa ofisi ya uongozi wa mambo ya uchumi na fedha ya China Bw. Yang Weimin leo amesema, mapendekeo yaliyopitishwa hivi karibuni kuhusu mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano yameweka ongezeko la asilimia 6.5 kuwa matarajio ya msingi, na sio lengo la uchumi wa China katika miaka mitano ijayo, na lengo halisi la ongezeko litatangazwa rasmi mwezi Machi mwaka kesho. Bw. Yang Weimin anasema,

    "nimeona kwamba hivi karibuni kuna watu wanaozungumzia ongezeko la asilimia 6.5. Lakini hii ni makadirio ya msingi, na sio lengo. Kwa sababu kwa mujibu wa utaratibu wa taifa wa kuweka mipango, kwanza serikali kuu inatoa mapendekezo, halafu Baraza la serikali litatoa mwongozo wa mpango na hatimaye kuuwasilisha kwenye mkutano wa Bunge la umma la China utakaofanyika mwezi Machi mwaka kesho. Naamini kuwa lengo litakaowekwa litazingatia matakwa ya kutimiza ongezeko la maradufu la thamani ya jumla ya uchumi wa China na matarajio ya msingi ya ongezeko la asilimia 6.5, lakini kasi hiyo yenyewe sio lengo, lengo halisi litajulikana tu mwezi Machi mwaka kesho."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako