• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China afanya mazungumzo na wataalamu na viongozi wa kampuni kubwa kuhusu hali ya uchumi ya sasa

    (GMT+08:00) 2015-11-11 16:12:47

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang Jumatatu wiki hii amekutana na wataalamu na viongozi wa kampuni kubwa za China, na kusikiliza maoni na mapendekezo yao kuhusu hali ya uchumi ya sasa.

    "kwa sasa tunaweza kupata picha kamili, kuhusu hali ya sasa ya uchumi, haswa kwa mwaka huu mzima. Mwelekeo wa uchumi katika mwaka kesho utakuwaje? sasa pia tumeanza kuweka mpango. Kwa hiyo, kama kawaida, tunafanya mkutano huu na wataalamu na wajasirimali, na kusikiliza maoni na mapendekeo yenu."

    Hii ni mara ya tatu kwa Bw. Li keqiang kufanya mazungumzo kama hayo na wataalamu wa uchumi na viongozi wa kampuni kubwa baada ya kufanyika kwa mikutano ya bunge na baraza la mashauriano ya kisiasa kwa mwaka. Tofauti na zamani, mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa mwaka, si kama tu unatakiwa kujumuisha uzoefu wa mwaka jana mzima, na bali pia unatarajiwa kuweka mipango kwa ajili ya mwaka kesho.

    Maoni ya wajasiriamali mara kwa mara yanampatia waziri mkuu huyo mawazo mapya, na pia atatoa mapendekezo yake kwa ajili ya uvumbuzi wa kampuni zao.

    "Unaweza kuwasiliana na kampuni ya Metersbonwe, vifaa vya elektroniki vya kuvaa vinaweza kushirikiana na sekta ya nguo, kufanya hivyo kunaweza kuvumbua bidhaa mpya, na pia kunaweza kuendana na mahitaji mapya katika soko. Sina nia ya kulazimisha ushirikiano huu, mnaweza kujadiliana baadaye. Mliyosema yanaonesha mna wazo la pamoja. Ulisema unapanga kuongeza mapato mwaka kesho, kutimiza lengo hili kunahitaji nafasi mpya ya ongezeko, unapaswa kuvumbua utoaji mpya kwenye soko."

    Na kuhusu hali ya uchumi wa China katika siku za baadaye, Bw. Li Keqing anasema:

    "Kwenye mkutano wa 5 wa kamati kuu ya 18 ya chama cha kikomunisti cha China uliomalizika hivi karibuni, tumetoa mapendekezo ya kuweka mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano, lengo kuu ni kukamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora ifikapo mwaka 2020. Wakati huo, pato la jumla la taifa GDP la China kwa kila mtu linatarajiwa kuwa dola za kimarekani elfu 12. Lazima tuwe na nia thabiti ya kufanikisha lengo hilo. Aidha, pia tunapaswa kufanya tathmini kamili kuhusu matatizo na changamoto zinazoweza kutukabili."

    Bw. Li Keqiang pia amesisitiza umuhimu wa uvumbuzi katika ukuaji wa uchumi.

    "Tunapaswa kuchochea zaidi nguvu ya uhai katika soko na nguvu ya uvumbuzi katika jamii. Mkutano wa 5 wa kamati kuu ya chama umedhihirisha wazi umuhimu wa uvumbuzi, ambao unachukua nafasi ya kwanza katika malengo ya maendeleo katika pande tano. Tumesisitiza mara kwa mara kwamba kuhimiza uvumbuzi kunatakiwa kupewa hadhi muhimu kwenye mkakati wa taifa. kwa kweli, uvumbuzi haumaanishi uvumbuzi wa teknolojia tu, bali pia unamaanisha uvumbuzi kwa mfumo, ambao unapatikana tu kwa njia ya mageuzi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako