• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa 13 wa miaka mitano wa China watoa fursa kwa maendeleo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2015-11-12 09:17:15

    Mshauri wa serikali ya China Yang Jiechi amesema, mpango wa 13 wa miaka mitano wa China unatoa fursa kwa ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa Serikali za Mitaa kati ya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing, Yang amesema mpango huo wa maendeleo wenye dhana ya uvumbuzi, uratibu, kijani, wazi, na kushirikisha wote unatoa fursa ya ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika.

    Akizungumza kwa niaba ya wajumbe kutoka Afrika, waziri wa serikali za mitaa na maendeleo ya miji na vijiji nchini Zimbabwe Saviour Kasukuwere amesema, uchumi wa Afrika umeendelea kwa kasi kutokana na uwekezaji wa China na ujenzi wa miundombinu, mikopo ya upendeleo na mafunzo.

    Wakati huohuo, balozi wa China nchini Zambia Yang Youming amesema, China na Afrika zinatakiwa kutumia mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mwezi ujao mjini Johannesburg, Afrika Kusini, kuimarisha uhusiano wa kimaendeleo kati yao katika sekta mbalimbali. Katika makala yake iliyochapishwa kwenye gazeti la Daily Mail la Zambia, Yang amesema pande hizo mbili zinatakiwa kutumia vizuri fursa ya mkutano huo ili kuendeleza zaidi ushirikiano wa Kusini-Kusini ili ufikie kwenye ngazi mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako