• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mitaji ya nje inayowekezwa nchini China yaongezeka kwa utulivu katika miezi 10 iliyopita

    (GMT+08:00) 2015-11-12 16:53:04

    Katika miezi 10 iliyopita, mitaji ya kigeni inayowekezwa nchini China imeongezeka kwa utulivu, na imetumiwa zaidi kwenye sekta ya huduma za teknolojia ya juu na viwanda. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, ingawa ongezeko la biashara ya China na nje limepungua, lakini China pia imedumisha nafasi yake ya kwanza kwa ukubwa wa biashara duniani.

    Mkurugenzi wa idara ya uwekezaji kwa nje katika wizara ya biashara ya China Bw. Tang Wenhong jana alisema, katika miezi ya 10 iliyopita ya mwaka huu, mitaji ya nje inayowekezwa nchini China imeendelea kuongezeka.

    "Kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu, mitaji ya kigeni inayowekezwa nchini China imedumisha ongezeko la utulivu, idadi ya makampuni mapya yaliyoanzishwa kwa ajili ya uwekezaji wa nje imefikia 21,022, ambayo ni ongezeko la asilimia 9.3, thamani ya mitaji ya nje iliyotumika ni yuan bilioni 639.42, ambayo imeongezeka kwa asilimia 8.6 kuliko mwaka jana muda kama huo. Kwa mwezi Oktoba pekee, makampuni mapya 2,042 yanayo wekeza nje yalianzishwa kote nchini China, ambayo ni ongezeko la asilimia 2.5 kuliko mwaka jana muda kama huo."

    Tofauti na hali ya uwekezaji wa nje nchini China, mwaka huu hali ya biashara ya China na nje si ya kufurahisha. Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na idara kuu ya forodha ya China zinaonesha kuwa, katika miezi 10 ya mwanzo mwaka huu, thamani ya jumla ya biashara ya China na nje ni yuan trilioni 19.93, ambayo imepungua kwa asilimia 8.1 kuliko mwaka jana muda kama huu. Wachambuzi wanaona kuwa, mwelekeo huo huenda ukaendelea mpaka mwishoni mwa mwaka huu.

    Lakini, naibu mkurugenzi wa idara ya biashara na nje katika wizara ya biashara ya China Bw. Wang Dongtang amesema, ingawa takwimu si za kufurahisha, lakini China bado imedumisha nafasi ya kwanza kwa ukubwa wa biashara duniani. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, biashara ya uuzaji nje ya China iko katika hali nzuri zaidi kuliko nchi nyingine kubwa na nchi za masoko mapya, thamani ya biashara ya uuzaji nje ya China imechukua asilimia kubwa zaidi katika ile ya jumla duniani.

    "Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, biashara ya uuzaji nje ya China imechukua asilimia kubwa zaidi katika ile ya jumla duniani. Inakadiriwa kuwa hivi sasa biashara ya uuzaji nje ya China inachukua asilimia 13 ya ile ya dunia nzima, na ilikuwa ni asilimia 12.4 mwishoni mwa mwaka jana."

    Ofisa huyo pia amesema, muundo wa biashara ya uuzaji nje ya China umeendelea kuboreshwa, uuzaji wa vifaa na ushirikiano wa uzalishaji viwanda umetoa motisha mpya kwa biashara ya uuzaji nje ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako