• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mauzo ya siku ya makapera kupitia tovuti ya Tmall ya Alibaba yaongezeka kwa asilimia 60

    (GMT+08:00) 2015-11-12 18:18:43

    Mauzo ya siku ya makapera kupitia tovuti ya Tmall unaomilikiwa na kampuni kubwa ya biashara kupitia internet ya China Alibaba yamefikia dola za kimarekani bilioni 14.3 mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 60 ikilinganishwa na mwaka jana.

    Data za kampuni hiyo zimeonyesha kuwa, zaidi ya asilimia 68 ya mauzo yalifanyika kupitia njia za kisasa kama vile simu za mkononi za kisasa na tablets.

    Taarifa zilizotolewa na makao makuu ya kampuni hiyo mkoani Zhejiang, mashariki mwa China imesema, nchi na sehemu 232 zimeshiriki kwenye mauzo hayo, ikiwa ni pamoja na chapa zaidi ya 5,000 kutoka nchi za nje. Nchi zilizoongoza katika mauzo hayo kwa upande wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi ni Marekani, Japan, Korea Kusini, Ujerumani, na Australia.

    Wakazi wa vijijini pia walishiriki kwenye punguzo hilo katika vituo zaidi ya 8,000 vilivyowekwa na kampuni hiyo ambavyo vilitoa huduma ya mtandao wa internet bila malipo. Wakazi hao walinunua mablanketi ya manyoya, nguo za ndani, pamoja na mashine za kufulia nguo.

    Bidhaa maarufu za dijitali zilizonunuliwa kwa wingi ni simu za mkononi aina ya iPhone na televisheni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako