Mjumbe wa kudumu wa China katika ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva na katika mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswisi Bw. Wu Hailong jana alimkabidhi mkurugenzi mkuu wa Shirika la leba la kimataifa ILO waraka wa kuidhinisha Mkataba wa kazi kuhusu mambo ya bahari wa mwaka 2006 uliopitishwa na China. Bw. Wu amesema, China itatekeleza kwa makini wajibu mbalimbali wa mkataba huo, pia itanufaishwa kikamilifu na haki mbalimbali zinazotolewa na mkataba huo, ili kuhimiza maendeleo ya mambo ya usafari baharini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |