Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China leo imesema, ili kuhimiza mageuzi ya uchumi na kuongeza ufanisi wake, China itaharakisha maendeleo ya sekta ya utoaji huduma, kulingana na mahitaji mapya ya matumizi, ili kuendeleza utoaji mpya sokoni na kukuza msukumo mpya wa uchumi.
Hivi karibuni Baraza la serikali la China lilipitisha nyaraka mbili kuhusu kukuza utoaji mpya wa soko na msukumo mpya wa uchumi kutokana na mahitaji mapya ya soko, na kuharakisha maendeleo ya sekta ya utoaji huduma.
Naibu mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Lin Nianxiu amesema, kutekelezwa kwa nyaraka hizo mbili kutasaidia kuhimiza mageuzi ya uchumi na kuongeza ufanisi wa uchumi, na pia kutaboresha maisha ya watu na kuongeza nafasi za ajira.
"Nyaraka hizi zimetilia maanani maeneo 10 ambayo yanahusiana kwa karibu na maisha ya watu, yana mahitaji makubwa ya soko na kuweza kutoa msukumo mpya kwa uchumi, ikiwemo wakazi, familia, afya ya umma, huduma kwa wazee, utalii, michezo, utamaduni, sheria, biashara ya jumla na ya rejareja, hoteli na mikahawa, elimu na mafunzo na kadhalika. Nyaraka hizo zimeweka bayana majukumu ya mendeleo katika maeneo hayo 10."
Mahitaji ya sokoni yakiwa ni injini muhimu ya ongezeko la uchumi, kuboresha muundo wa matumizi si kama tu kumeonesha mabadiliko makubwa katika muundo wa uchumi, bali pia kutasukuma mbele maendeleo ya sekta husika. Kuhusu hali hiyo, Baraza la serikali la China pia limesema, China inapaswa kutumia nafasi ya uongozi wa matumizi mapya, katika kupanua utoaji wa sokoni, kuhimiza uvumbuzi kwenye mfumo, kuboresha mazingira ya matumizi na kuboresha mfumo wa sera.
Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2014 thamani ya matumizi ya watu wa China katika nchi za nje imefikia yuan trilioni moja. Wachambuzi wanaona kuwa, tofauti katika bei na sifa ni sababu kuu ya hali hiyo. Mkurugenzi wa idara ya mipango katika kamati ya maendeleo na mgeuzi ya China Bw. Xu Lin amesema, katika siku zijazo, China itaendelea kurahisisha utaratibu wa kuingiza bidhaa kutoka nje, hatua zitakazochulikuwa ni pamoja na kuongeza idadi ya maduka yasiyotozwa ushuru, kutekeleza na kukamilisha utaratibu wa kurudisha kodi wa watalii wanapoondoka nchini.
"Ili kukidhi mahitaji ya matumizi ya wananchi, tutarahisisha zaidi utaratibu wa kuingiza bidhaa kutoka nchi za nje, na kuongeza idadi ya maduka yasiyotozwa ushuru, ili kuwawezesha wateja wa China na wa nje wanunue bidhaa nyingi zaidi zilizoagizwa kutoka nje. Hatua hizo zitatekelezwa baada ya kutolewa kwa nyaraka hizo."
Takwimu zinaonesha kuwa, matumizi yamekuwa nguvu muhimu ya msukumo kwa uchumi wa China. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, matumizi yamechangia asilimia 60 ya ongezeko la uchumi, ambayo ni ongezeko la asilimia 5.7 kuliko mwaka jana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |