Uwekezaji huo ni wa makampuni zaidi ya elfu 5 ya China yaliyokuwepo katika nchi na sehemu 152 duniani.
Naibu mkurugenzi wa ofisi ya uwekezaji kwa nje katika wizara ya biashara ya China Bw. Jiang Wenbin amesema miradi ya nje kama vile usafiri, ujenzi wa nyumba, umeme, na mawasiliano ya simu iliyosainiwa iliongezeka kwa kiasi kikubwa, na thamani ya jumla ya miradi hiyo inazidi dola bilioni 108 za kimarekani.
Takwimu hizo pia zinaonesha kwamba uwekezaji wa China katika sekta ya utengenezaji umeongezeka kwa asilimia 82, na utengenezaji wa simu za mkononi, mashine, kompyuta, vifaa vya mawasiliano zimewekezwa zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |