Baada ya serikali ya China kutoa mpango wa kupambana na bidhaa feki zinazouzwa nje ya nchi, idara mbalimbali za China zimechukua hatua kwa pamoja za kupambana na bidhaa feki ili kulinda sifa ya "Made in China".
Kwa mujibu wa mpango huo, China itachukua hatua mbalimbali za kuongeza udhibiti wa ubora wa bidhaa na kulinda sifa ya bidhaa za China. Bw. Chai Haitao, ni naibu mkurugenzi wa idara inayoongoza kampeni hiyo.
Sauti-1
"hatua ya kwanza ni kudhibiti chanzo cha bidhaa feki kwa kuimarisha usimamizi wa uingiaji wa bidhaa sokoni. Ya pili ni kusafisha masoko makuu, na ya tatu ni kuongeza usimamizi wa bidhaa zitakazouzwa nje ya nchi, ambapo idara ya forodha inaongeza ukaguzi katika sehemu ya utengenezaji na bandari ambayo kesi ya bidhaa feki zinakutwa kwa wingi. Ya nne, ni kuiwekea kanuni biashara ya kuvuka mipaka kupitia mtandao wa Internet, na ya tano ni kuzidisha ushirikiano wa kimataifa."
Ofisa kutoka mamlaka ya usimamizi wa ubora wa bidhaa ya China Bw. Liu Shiyuan amesema ubora wa bidhaa zinazokwenda Afrika utaangaliwa zaidi.
Sauti-2
"katika miezi 10 ya kwanza ya mwaka huu, idara yetu imekamata shehena zaidi ya 4000 za bidhaa za hali duni zilizokuwa zinauzwa barani Afrika, na kuzuia shehena zaidi ya 13,00. Kiasi hiki kilipungua kikilinganishwa na kile cha mwaka jana. "
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |