Kazi hiyo ya uwekezaji ilianza jana, na lengo lake ni kuongeza biashara na kuimarisha mahusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Shughuli hii pia utumika kama fursa nzuri kwa nchi ya Afrika Kusini kwa kusaidia nchi hiyo kupata fursa ya kuuza bidhaa zake nchini ugunda.
Ujumbe huo wa biashara utashiriki katika mikutano mbalimbali ya kibiashara, watatembelea semina za biashara na uwekezaji.
Balozi wa Afrika Kusini nchini Uganda, Generali Lekoa Mollo, anasema jumuiya ya biashara Uganda iko tayari kufanya biashara na Afrika Kusini, na imeonnyesha nia ya kushirikiana na kufanya kazi katika sekta mbalimbali ambazo zinaweza kufaidika nchi zote mbili.
Aidha anasema OSIM pia itaunganisha sekta binafsi kutoka Afrika Kusini na sekta binafsi nchini Uganda kwa matumaini ya kuongeza fursa za biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |