China imechukua hatua kubwa ya kufanya elimu ya msingi iwe ya haki zaidi kwa watu wote, baada ya Baraza la Serikali kuamua fedha zitakazotolewa na serikali kwa shule za vijijini au zile za watoto wa wafanyakazi wahamiaji, zitakuwa sawa na zile zinazotolewa kwa shule za mijini. Wataalamu wamekadiria kuwa hatua hiyo itaifanya serikali kutumia dola bilioni 2.35 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa Baraza la Serikali ulioendeshwa na waziri mkuu wa China Bw Li Keqian, imesema serikali itaweka kiwango sawa cha msingi kwa shule zote kuanzia mwaka kesho, na kuanzia mwaka 2017 ada na gharama za vitabu kwa elimu ya lazima zitaondolewa kabisa, na wanafunzi kutoka familia maskini watapatiwa ruzuku.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |