• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa lataka kuinua uwezo wa matibabu

    (GMT+08:00) 2015-11-25 17:11:15

    Shirika la kupambana na UKIWMI la Umoja wa Mataifa UNAIDS jana huko Geneva lilitoa ripoti ya maambukizi ya UKIMWI kwa mwaka 2015. Ripoti hiyo inazitaka nchi mbalimbali zijitahidi kutekeleza "mkakati wa njia ya haraka" wa shirika hilo ili idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ambao wanapata matibabu waongezeke maradufu hadi kufikia mwaka 2020.

    UNAIDS limenatoa ripoti hiyo kila mwaka, kwa ajili ya kufanya uchambuzi kwa mwelekeo wa maambukizi ya UKIMWI na kuelekeza nchi mbalimbali kuweka hatua zenye ufanisi zaidi. Katika mkutano na waandishi wa habari, mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bw. Michel Sidibe amesema, ripoti ya mwaka huu ina tofauti kubwa na ripoti za zamani.

    "katika miaka 30 iliyopita, tumetoa ripoti hiyo kila mwezi Desemba, ambayo inajumuisha hali ya maambukizi ya UKIMWI. Katika ripoti ya mwaka huu, tunataka kuwafahamisha watu umuhimu wa jamii katika kukabiliana na UKIMWI. Tunaweza kuchukua hatua gani na vipi hatua za kimkakati zinaweza kutusaidia kuboresha utekelezaji wa kukabiliana na UKIMWI. "

    Bw. Michel Sidibe amesema kutokana na nchi mbalimbali kutekeleza mkakati wa njia ya haraka uliotolewa na UNAIDS, binadamu wamepata maendeleo makubwa katika kukabiliana na ugonjwa wa UKIMWI. Hadi kufikia mwezi Juni mwaka 2015, watu milioni 15.8 walioambukiza UKIMWI wamepata tiba ya antiretroviral, na idadi hiyo ya mwaka 2010 ni milioni 7.5, na mwaka 2005 ni milioni 2.2 tu. Aidha, idadi ya watu wanaoambukiza UKIMWI imepungua kwa asilimia 35 kuliko mwaka 2000 ilipokuwa kiwango cha juu kabisa. Bw. Sidib amesema,

    "Matokeo ya uchambuzi wa ripoti hiyo yanavutia. Kila baada ya miaka mitano, idadi ya watu wanaopata matibabu inaongezeka maradufu. Kweli inatushangaza. Kama ukikumbuka mwaka 1996 hakukuwa na mtu anayepata matibabu. "

    Tiba ya antiretroviral inachukuliwa kuwa na matibabu yenye ufanisi zaidi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa sasa, inaweza kurefusha maisha ya wagonjwa na kuinua ubora wa maisha ya wagonjwa. Kwa hivyo shirika la UNAIDS linapendekeza kuwa, mtu akithibitisha kuambukizwa, ni lazima aanze kutumia tiba ya antiretroviral mara moja. "Mkakati wa njia ya haraka" ni kwamba inapaswa kuinua kiwango cha matibabu ya UKIMWI kwa haraka kote duniani, hasa katika sehemu zenye hali mbaya ya maambukizi zinapaswa kuchukua hatua kwa haraka. Kwa sasa, nchi mbalimbali zinafanya juhudi kubwa, ili idadi ya watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI ambao wanapata matibabu waongezeke maradufu hadi kufikia mwaka 2020. Bw. Sidibe ana imani kubwa na kinga na tiba ya UKIMWI.

    "kama umekwenda Afrika, utaona kuwa zamani wagonjwa walifariki bila matumaini yoyote, hata wagonjwa waliolazwa wodini pia walikata tamaa. Leo watu wanaona, tunaelekea kwenye matumaini kutoka kukata tamaa. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako