• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WMO yasema, 2015 ni mwaka wa joto kali zaidi katika historia

    (GMT+08:00) 2015-11-26 20:32:10

    Ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani WMO imesema 2015 utakuwa ni mwaka wa joto kali zaidi katika historia.

    Katibu mkuu wa shirika hilo Michel Jarrau amesema, hali ya hewa duniani katika mwaka huu ni ya kihistoria.

    "katika sehemu nyingi duniani kumekuwa na rekodi mpya za joto kali. Mabara ya Ulaya, Amerika ya Kusini na Oceania yameweka rekodi ya joto kali, na Afrika imekuwa nafasi ya pili kwa kuwa na joto kali, karibu sehemu zote duniani zimevunja rekodi."

    Ripoti hiyo inasema joto hilo linasababishwa na matukio ya El Nino na ongezeko la joto duniani linalotokana na shughuli za binadamu. Tathmini ya kisayansi inaonyesha kuwa, kutokana na mabadiliko ya hewa yaliyosababishwa na shughuli za binadamu, uwezekano wa kutokea kwa hali mbaya ya hewa duniani umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Bw. Michel amesema,

    "hizi si habari nzuri. Katika halijoto ya dunia, na suala la hali mbaya ya hewa na utoaji wa Cabon dioxide, tunatumai kuwapatia habari hizo wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa, na tunatarajia wataweza kutambua ulazima wa kufikia makubaliano."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako