• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Didier Drogba kuwa kocha wa Chelsea

    (GMT+08:00) 2015-11-27 09:51:02

    Mshambulizi wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amesema kuwa atarejea Stamford Bridge kuwa kocha.

    Drogba, mwenye umri wa miaka 37 ambaye kwa sasa anasakata soka ya kulipwa huko Canada, aliifungia the Blues mabao 164 katika enzi yake huko Stamford Bridge.

    Amesema kwamba tayari amekubaliana na wakurugenzi wa klabu hiyo kuwa anaweza kurejea kuwa mkufunzi.

    Drogba ndiye aliyeifungia Chelsea bao lililoipa ushindi na taji la mabingwa wa bara Ulaya mwaka wa 2012.

    Vilevile aliisaidia Chelsea kunyakwa mataji 4 ya ligi kuu ya Uingereza kabla ya kuhamia Canada kujiunga na Montreal Impact.

    Chelsea haijakuwa na mwanzo mzuri katika msimu huu baada ya kushindwa katika mechi 7 kati ya 12 za kwanza msimu huu.

    Mabingwa hao watetezi wanashikilia nafasi ya 15 katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako