• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakadiriwa kuendelea kuongoza duniani kwa kuuza zaidi bidhaa nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2015-11-27 09:54:02
    Ripoti kuhusu mustakbali wa biashara duniani iliyotolewa jana na Benki ya HSBC inasema, China itaendelea kuongoza duniani kwa kuuza bidhaa nje kwa wingi. Ripoti hiyo inasema kutokana na ujio wa raundi ya tatu ya wimbi la utandawazi duniani unaohimizwa na teknolojia mpya na maingiliano ya kiuchumi, biashara duniani imeingia kwenye kipindi kipya, na ustawi wa biashara barani Asia utaongoza ukuaji wa biashara duniani, na kuhimiza thamani ya jumla ya uuzaji bidhaa nje duniani kuongezeka kwa mara nne ifikapo mwaka 2050, na kufikia dola za kimarekani trilioni 68.5.

    Ripoti hiyo inaongeza kuwa kutekelezwa kwa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na kuundwa kwa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia, AIIB, kutachangia ukuaji zaidi wa biashara nchini China, na hadi kufikia mwaka 2050 thamani ya bidhaa za China zinazouzwa nje ya nchi inatarajiwa kuwa karibu dola za kimarekani trilioni 12.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako