• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza uwekezaji barani Afrika

    (GMT+08:00) 2015-11-27 10:18:10

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw Qian Keming amesema China itaongeza uwekezaji barani Afrika na kununua bidhaa nyingi zaidi zisizo maliasili kutoka Afrika, na pia itaziuzia nchi za Afrika zana za kisasa kwa ajili ya kuhimiza uzalishaji.

    Akiongea kuhusu mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika unatarajiwa kufanyika wiki ijayo huko Afrika Kusini, Bw Qian amesema, kwenye mpango huo China itatoa mapendekezo mapya kuhusu maeneo ya ushirikiano. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuzisaidia nchi za Afrika kuboresha muundo wa viwanda, kulinda usalama wa chakula na ujenzi wa miundo mbinu.

    Wakati mkutano wa kilele wa kujadili na kupitisha mapendekezo hayo ukisubiriwa, jana mkutano wa wanasheria wa Afrika na China ulifanyika mjini Johannesburg, na mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Chama cha Sheria cha China inayoshughulikia mawasiliano na nje Daktari Gu Zhaomin amesema kwenye mkutano huo kuwa China iko tayari kubadilishana ujuzi na uzoefu wake na nchi za Afrika. Bw Gu amesema China na nchi za Afrika zinatakiwa kutumia baraza la wanasheria kusaidia kufanikisha uwepo wa ushirikiano wa kunufaisha na mustakbali wa pamoja kati ya China na Afrika.

    Wanasheria hao pia wameanzisha kituo cha utatuzi wa migogoro kati ya China na Afrika, kitakachokuwa mbadala wa mahakama katika kutatua mgogoro kati ya pande mbili. Mwanasheria wa Afrika Kusini Bw Michael Kuper amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza wa kituo hicho. Kituo hicho kimeanzishwa kutokana na kuongezeka kwa migogoro ya kibiashara kati ya China na nchi za Afrika na mchakato wa polepole wa mahakama kushughulikia migogoro hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako