• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajitahidi kujiendeleza bila ya uchafuzi

    (GMT+08:00) 2015-12-24 15:31:00

    Mwezi Septemba mwaka huu, mbuga kubwa ya kwanza ya taifa ya wanyama pori nchini China, yaani Mbuga ya taifa ya Paa wa kitibet na ng'ombe pori ya Qiangtang mkoani Tibet ilianzishwa huko Lhasa, na jumla ya eneo hili la hifadhi ya kimaumbile imefikia kilomita laki 2.98 za mraba, ambayo inasifiwa kama peponi ya wanyama pori. Mfanyakazi wa kushughulikia uhifadhi wa wanyama pori wa Naruotang Kajiadama amesema,

    "Zamani katika Naruotang, idadi ya Paa wa kitibet kwa wingi ilikuwa 30 au 40, lakini sasa kutokana na juhudi za idara ya misitu za kuwalinda Paa hao, katika msimu wa kuzaliana, idadi ya Paa inafikia zaidi ya elfu moja, tena Paa wa hapa Naruotang hawahami kamwe, hivyo idadi yake inaongezeka kwa haraka."

    Sio tu Paa wa kitibet, katika miaka ya hivi karibuni, kadiri nguvu za kuwalinda wanyama pori inavyoimarishwa, ndivyo idadi ya wanyama pori katika mbuga ya Qiangtang inaongezeka kwa kiasi kikubwa, na wanyama pori wengi adimu walioko katika hatari ya kutoweka kama vile Paa wa kitibet, ng'ombe pori, punda pori wa kitibet na chui wa maeneo yenye theluji wanaonekana katika maeneo mbalimbali.

    Imefahamika kuwa, eneo la jumla la hifadhi mbalimbali zilizopo sasa nchini China zikiwemo sehemu za vivutio, hifadhi za kimaumbile, bustani ya msitu, bustani ya kijiolojia, maeneo yenye michezo ya majini limefikia kilomita za mraba milioni 1.7, ambalo limechukua asilimia 18 ya eneo la jumla la ardhi ya China, na hilo ni ardhi nzuri zaidi nchini china.

    Mazingira ya asili ni msingi wa kuishi na kujiendeleza kwa binadamu. Kadiri jamii na uchumi vinavyoendelezwa, kuchafuka kwa mazingira kumekuwa suala ambalo China haiwezi kulipuuza, na kuhifadhi mazingira, kupunguza uchafu na kuzuia hali ya kiikolojia isiendelee kuwa mbaya kunatiliwa maanani sana na kuwekwa kipaumbile na china, na kujenga mbuga za taifa kumekuwa moja ya hatua nyingi za China za kuhifadhi mazingira.

    Mkutano wa 5 wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 18 Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu ulijadili na kupitisha Pendekezo la kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kutunga mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano. Kwenye pendekezo hilo, maendeleo bila uchafuzi yamekuwa moja ya mawazo matano makuu kuhusu maendeleo ya China katika miaka mitano ijayo. Pendekezo hilo limesema, China ikitaka kujiendeleza bila kuchafua mazingira, ni lazima ifuate dira ya kubana matumizi ya maliasili na kuhifadhi mazingira, na kuharakisha kujenga jamii inayobana matumizi ya maliasili na kuhifadhi mazingira. Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa sera za mazingira na uchumi katika wizara ya kuhifadhi mazingira ya China Xia Guang anaona kuwa, katika miaka mitano ijayo, maendeleo bila uchafuzi yatakuwa mwelekeo wa maendeleo ya China. Anasema,

    "Mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano ni kama ramani, namna ya kuuwekea ujenzi wa ustaarabu wa kiviumbe katika hadhi muhimu zaidi ya kimkakati, na namna ya kuufanya ujenzi huo uunganishwe na ujenzi mwingine, ndiyo roho ya mpango huo. Katika mpango huo, maendeleo bila ya uchafuzi ni kama msingi, hivyo tunaweza kusema mpango huo ni wa kisasa hata katika dunia nzima."

    Baada ya kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, wakati huo China haikuwa na uzoefu kabisa, hivyo ilifanya majaribio kupiga hatua, na kuendeleza kwa haraka uchumi wake tu, kwa hiyo baada ya miaka zaidi ya 30, uchumi wake umeongezeka kwa kasi, lakini mazingira ya asili pia yameharibiwa vibaya. Bw. Xia Guang amesema,

    "Zamani tulithamini maendeleo tu bila kuzingatia maliasili na mazingira, ingawa kweli tumepata maendeleo kwa kiasi, lakini hayalingani na matakwa ya ustaarabu wa kiviumbe, hivyo safari hii tumeongeza matakwa ya maendeleo bila ya uchafuzi, ili kutimiza lengo la kupata maendeleo bila kuchafua mazingira. Hii inaonesha kuwa mwongozo wetu wa jumla wa thamani kuhusu maendeleo ni wazi zaidi, na pia inalingana zaidi na lengo la muda mrefu."

    Baada ya mwaka 2013, uchumi wa China uliingia katika "hali mpya ya kawaida", yaani ongezeko la uchumi limepungua, huku muundo wa uchumi umeboreshwa, na uchumi unaendelezwa kwa uvumbuzi sio uwekezaji. Naibu mkuu wa shirikisho la utafiti wa ustaarabu wa kiviumbe la China Bw. Zhu Guangyao amesema,

    "Tunatakiwa kuendana na matakwa ya sasa ya ustaarabu wa kiviumbe na kubadili njia ya maendeleo ya zamani, huu ni mchakato mgumu wa mabadiliko, kama hatuna nia kubwa ya kufanya mabadiliko, basi ni vigumu kuhimiza mabadiliko hayo, la muhimu ni kuwa na imani imara, na kushikilia maendeleo endelevu na maendeleo bila kusababisha uchafuzi, na tunaweza kutimiza malengo hayo."

    Mkoa wa Guangdong ulioko kusini mashariki mwa China unanufaishwa na wazo la maendeleo bila uchafuzi. Katika miaka miwili iliyopita, mazingira ya kiviumbe ya huko yameboreshwa kidhahiri. Habari zinasema uwezo wa mkoa huo wa kushughulikia maji taka umekuwa zaidi ya tani milioni 20 kwa siku, ambao unachukua asilimia 13 hivi ya ule wa kote nchini China. Kati ya mito 7 mikubwa nchini China, mazingira ya maji ya Mto Zhujiang ni mazuri zaidi, na mkoa huo pia umepata maendeleo katika udhibiti wa hewa chafu. Mkurugenzi wa shirika la ekolojia la China profesa Guan Dongsheng amesema,

    "Guangdong ni mkoa ambao thamani ya jumla ya uzalishaji GDP imechukua nafasi ya kwanza nchini China, hivyo una utoaji mkubwa wa jumla wa uchafuzi, na kazi yake ya kupunguza uchafuzi ni kubwa, lakini China inatoa fedha nyingi katika mambo ya kuhifadhi mazingira katika "mpango wake wa 13 wa maendeleo ya wa miaka mitano", hivyo Guangdong hakika inapaswa kutumia fursa hii kuendeleza shughuli za uhifadhi wa mazingira, ili kufanya vizuri zaidi kazi ya kuhifadhi mazingira."

    Kadiri maendeleo ya jamii na uchumi, watu si kama tu wanahitaji maisha ya utajiri bila kuwa na wasiwasi kuhusu nguo na chakula, mazingira mazuri pia ni kigezo cha maisha ya watu yenye furaha. Kuishi na mazingira ya asili kwa mapatano na maendeleo bila ya uchafuzi ni mambo yanayofuatiliwa zaidi nchini China kwa sasa na katika siku za usoni. Wazo hilo la China la kutilia maanani uhifadhi wa mazingira na kupendekeza maendeleo endelevu linasifiwa na watu kutoka nchi za nje. Waziri mkuu wa zamani wa Italia Bw. Mario Monti amesema,

    "Naona ni bora kuwa maendeleo ya uchumi wa China au wa dunia, uwiano ni jambo muhimu la maendeleo endelevu, hivyo naona China kwa sasa kuweka mkazo katika kuhifadhi mazingira wakati inapoendeleza uchumi ni muhimu sana, na hatua hii itasaidia China kuwa na uwiano zaidi katika maendeleo ya uchumi na uhifadhi wa mazingira."

    Kuanzia tarehe 30 Novemba hadi tarehe 11 mwezi huu, Mkutano wa 21 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ulifanyika huko Paris, Ufaransa. Rais Xi Jinping wa China alihudhuria ufunguzi wake, ambapo kwenye hotuba yake alifahamisha dunia nzima wazo na mpango wa China wa "kushughulikia kwa makini mabadiliko ya hali ya hewa". Katika mchakato wa kuhimiza nchi mbalimbali duniani kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, China inageuka kuwa mjenzi anayefanya juhudi kutoka mshiriki wa zamani. Rais Xi amesema,

    "Katika 'waraka wa kutoa mchango katika mabadiliko ya hali ya hewa', China imebainisha kuwa hadi kufikia mwaka 2030 utoaji wa hewa ya carbon wa China utafika kileleni, na itafanya juhudi kutimiza lengo hilo mapema, na mwaka 2030 kupunguza utoaji wa hewa ya carbon wa kila GDP kwa asilimia 60 hadi 65 kulingana na kiwango cha mwaka 2005, na ongezeko la misitu kuongezeka kwa mita za ujazo bilioni 4.5. Ingawa tunapaswa kufanya juhudi kubwa, lakini tuna imani na tuna nia kutimiza ahadi zetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako