• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya mwaka 2015 kuhusu pengo la kijinsia duniani

    (GMT+08:00) 2015-12-29 08:58:03

    Kongamano la uchumi duniani lililofanyika mjini Geneva hivi karibuni lilitoa Ripoti ya mwaka 2015 kuhusu pengo la kijinsia duniani, ambayo inaonesha kuwa katika miaka 10 iliyopita, pengo la jumla kati ya wanaume na wanawake duniani katika upande wa afya, elimu, nafasi za kiuchumi na nafasi za kushiriki kwenye shughuli za kisiasa limepungua kwa asilimia 4, huku pengo la kiuchumi likipungua kwa asilimia 3 tu.

    Ripoti ya pengo la kijinsia duniani ilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2006. Na ripoti ya mwaka huu imetoa tathmini kwa nchi 145 duniani katika upande wa kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi, elimu, kupewa haki za kisiasa, afya na kuishi. Matokeo husika yanaonesha kuwa katika miaka 10 iliyopita ingawa wanawake milioni 250 zaidi wameingia katika soko la nguvukazi, lakini kiwango cha nafasi za wanawake kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi bado kiko chini kuliko kile cha wanaume, pengo hili halijapungua, ongezeko la wanawake walioelimika halijainua kwa uwazi nafasi za kazi zao na mapato yao, thamani ya mapato ya wanawake katika mwaka 2015 ni sawa na yale ya wanaume katika miaka 10 iliyopita, na kama hali hiyo itaendelea, itachukua miaka 118 kuondoa kwa pande zote pengo la kiuchumi kati ya wanaume na wanawake.

    Katika orodha ya nchi zilizofanikiwa zaidi katika kutimiza lengo la kujipatia usawa wa kijinsia, nchi za kaskazini mwa Ulaya ziko mstari wa mbele, huku nchi tatu za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zikiingia katika nchi 20 za kwanza, miongoni mwa nchi hizo Rwanda iko nafasi ya 6.

    Mwezi Septemba mwaka huu, China imetoa waraka kuhusu usawa wa kijinsia na maendeleo ya wanawake, ikielezea kwa kina sera yake kuhusu wanawake. Waraka huo uliotolewa wakati wa maadhimisho ya miaka 20 tangu mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake ufanyike mjini Beijing unasema, usawa wa kijinsia na maendeleo ya wanawake nchini China sio tu unaonyesha mafanikio ya nchi hiyo, bali pia ni kama mchango uliotolewa kwa usawa wa kijinsia, maendeleo na amani duniani. Waraka huo unasema, mfumo wa kuinua hadhi ya wanawake nchini China unakamilika siku hadi siku, huku pengo kati ya wanaume na wanawake katika masuala ya elimu likipungua kwa kiasi kikubwa. Naibu mkurugenzi wa kamati ya kazi za wanawake na watoto katika baraza la serikali ya China Bibi Song Xiuyan amejulisha kuwa:

    "Mwaka 2013, idadi ya wanawake walioajiriwa ilichukua asilimia 45 ya idadi ya watu walioajiriwa kote nchini China. Mwaka 2014 kiwango cha kuelimishwa kwa watoto wa kiume na kike katika shule za msingi nchini China kilikuwa ni asilimia 99.8, ambapo malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa yalitimizwa kabla ya wakati. Na umri wa kuishi wa wanawake kwa wastani nchini China umerefushwa, ambao mwaka 2010 ulifikia miaka 77.4, huku uliongezeka kwa miaka 4.1 kuliko mwaka 2000, na umri huo ni miaka 5 zaidi kuliko ule wa wanaume."

    Mwanzilishi wa Kongamano la Uchumi Duniani Klaus Schwab amesema, mageuzi ya nne ya kiviwanda yanaongoza kiwango cha matumizi ya mitambo inayojiendesha duniani kuinuka kwa kasi. Wakati huu tunahitaji zaidi kuzidisha usawa wa kijinsia duniani, ili mitizamo na michango ya wanawake iheshimiwe kwa usawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako