• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Filamu mpya ya Kongfu "Master" yaonesha uhalisi wa jamii ya wastadi wa Kongfu

    (GMT+08:00) 2016-01-02 20:23:54

    Kwenye kipindi cha leo tunazungumzia filamu moja ya Kongfu iitwayo Master iliyoanza kuoneshwa hivi majuzi ambayo imevutia mashabiki wengi wa Kongfu nchini China. Mwongozaji wa filamu hiyo Bw. Xu Haofeng amesema, filamu hiyo inalenga kuadhimisha tabaka la wastadi wa Kongfu lililotoweka kwa kupitia kueleza hadithi za mashindano ya ustadi na undugu kati yao zilizotokea katika tabaka hilo mjini Tianjin karibu miaka mia moja iliyopita.

    Unayosikiliza sasa ni sehemu ya filamu hiyo. Filamu hiyo iliyopewa tuzo ya Golden Horse ya Taiwan, inazungumzia hadithi kuhusu mkufunzi wa Kongfu Bw. Chenshi aliyekwenda Tianjian kwa ajili ya kueneza ustadi wa kongfu yake ya Wing Chun kwenye sehemu za kaskazini mwa China. Ili kuweza kuishi kwenye jamii ya wastadi wa Kongfu mjini Tianjin, Bw. Chenshi alijaribu kufungua taasisi yake ya kufunza Kongfu, halafu akapata mwanafunzi wa kwanza Bw. Geng Liangcheng. Kwa mujibu wa kanuni za wastadi wa Kongfu, mwanafunzi huyo alitakiwa kushambulia na kuwashinda wastadi wa kongfu wa taasisi nane ili kuweza kujenga umaarufu wao mjini Tianjin. Kuanzia hapo, mkufunzi Chenshi na mwanafunzi wake Bw. Geng Liangcheng walijiingiza kwenye shughuli nyingi zilizotokana na ushindani wa Kongfu na wote walijitahidi kutimiza ndoto zao tofauti ambazo kwa mkufunzi ni kuenza kongfu yake ya Wing Chun na kwa mwanafunzi ni kujenga umaarufu wake kwenye jamii ya wastadi wa Kongfu. Hatma zao za pamoja zimeimarisha zaidi undugu kati yao.

    Akizungumzia tabaka la wastadi wa Kongfu Mwongozaji Xu Shaofeng amesema, walikuwa ni watu mashuhuri sana kwenye jamii ya China karne moja iliyopita. Kabla ya vita dhidi ya uvamizi wa Japan, China ilikuwa ni jamii yenye ncha nyingi, kila sekta ilikuwa inajiendeleza kwa kujitegemea na pia zinasaidiana wakati wa lazima, hali ambayo pia ni burasa ya kisiasa ya wachina. Bw. Xu Haofeng amesema, Baada ya kuanza kwa vita, jamii ya China ilibadilishwa kuwa yenye matabaka mawili tu, yaani wanajeshi na raia wanaozalisha vifaa kwa ajili ya jeshi, kwa hiyo tabaka la wastadi wa Kongfu lililokuwepo kwa miaka zaidi ya 20 likatoweka.

    Bw. Xu anaongeza kuwa mji wa Tianjin ulikuwa ni kituo kikubwa cha Kongfu nchini China, kwenye filamu hiyo si kama tu alijitahidi kuonesha mstadi mmoja wa Kongfu, na bali pia alitaka kuonesha muundo wa jamii ya wakati huo mjini Tianjin.

    Kuanzia mwaka 2008, Wing chun ilikuwa ni kaulimbiu ya filamu za kongfu nchini China, lakini wakati filamu hii ya Master ilipoanza kutengenezwa, filamu zinazohusu Wing chun zilianza kudidimia. Mwongozaji Xu Shaofeng amesema, anapenda kufanya mambo ambayo wengine wameanza kuacha, kwa sababu anajua anachofanya na pia anapenda changamoto.

    Filamu za Kongfu zilianzishwa miaka ya 20 ya karne iliyopita, na kustawi miaka ya 40 karne hiyo huko Hongkong baada ya kuingiza ustadi wa opera na uchawi. Bw. Xu amesema, Opera na uchawi zilikuwa ni vyanzo viwili vya filamu za kongfu za Hongkong, lakini zilishindwa kuleta uvumbuzi wowote na kufikia kilele chake cha mwisho mwaka 1992.

    Baada ya hapo, vijana wa China wamechoka kutazama filamu zile za kongfu zilizochanganywa na vitendo vya opera na uchawi, kwa hiyo filamu za magenge, mapigano na majanga za Hollywood zikapata fursa kuingia kwenye soko la sinema China. Hadi kufikia miaka ya 90 ya karne iliyopita, filamu za Hollywood zilikuwa zimetawala soko la sinema nchini China.

    Ili kujaribu kubadilisha sura ya kongfu na kuokoa filamu za kongfu, Bw. Xu Haofeng anashikilia kuonesha uhalisi wa kongfu kitendo kwa kitendo kwa njia ya mantiki.

    Bw. Xu Haofeng amesema, filamu hiyo Master pia imetoa heshima kwa Bruce Lee kwa kuiga sehemu ya filamu yake iitwayo A warrior's Journey iliyopigwa mwaka 1978.

    Akizungumzia mustakbali wa filamu za kongfu, Bw. Xu amekiri kwamba filamu za aina hiyo zimeenza kudidimia baada ya kustawi kwa miaka 20 iliyopita. Amesema, lengo la filamu Master si kujaribu kustawisha filamu za kongfu, bali ni kuonesha uhalisi wa jamii ya wakati ule.

    Bw. Xu ameeleza kwamba filamu Master si kuonesha moja kwa moja tu uhalisi wa jamii na upande mbaya katika utu wa binadamu, bali inajaribu kueleza mahusiano yenye utatanishi na matabaka kwenye jamii ya wastadi wa Kongfu.

    Ili kuonesha uhalisi wa Kongfu ya aina ya Wing Chun, mwongozaji Xu haofeng alijifunza kwa muda mrefu kongfu hiyo kutoka kwa mrithi wa Kongfu Wing chun.

    Wing chun ni aina ya kongfu ya jadi ya China iliyoanzishwa mkoani Fujian, kusini mwa China. Ustadi wa Wing chun unatilia maanani kuzuia mashambulizi na kujilinda kwa ufanisi na kwa haraka. Ikilinganishwa na kongfu za aina nyingine nchini China, Wing Chun inazingatia zaidi kumaliza mshambuliaji haraka iwezekanavyo. Kwa kawaida Wing chun inatumia ngumi na mateke tu, lakini pia ina ustadi maalumu wa kutumia silaha mbili yaani visu mapacha vya Bazhandao na fimbo.

    Mwezi Novemba mwaka 2014, Kongfu ya Wingchun iliodhoreshwa kuwa ni urithi wa kiutamaduni wa taifa la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako