• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sherehekea mwaka mpya pamoja na vijana wanaojitolea kufundisha Kichina nchini Romania

    (GMT+08:00) 2016-01-07 21:11:26

    Chuo cha Confucious katika chuo kikuu cha Bucharest nchini Romania kilianzishwa mwaka 2013, na watu wanaojitolea kufundisha kichina kwenye chuo kicho wote ni wanafunzi wa vyuo vikuu au watihimu wapya. Ingawa wana sababu mbalimbali za kujitolea kufanya kazi hiyo, lakini lengo lao ni moja, kuwafahamisha watu wa Romania kuhusu China na utamaduni wake. Bw. Li Zhao ambaye anasoma katika chuo kikuu cha Bucharest pia ni mmoja kati ya hao wanaojitolea. Anasema,

    "Chuo cha Confucious ni taasisi inayoeneza utamaduni wa China, na inafanya shughuli mbalimbali za kiutamaduni. Nikiwa mwanafunzi anayesoma hapa, kila mara wanapofanya shughuli kama hizo, najitolea kuwasaidia, nikaona mambo wanayofanya yana maana sana na yamenivutia, kwa kuwa yanabadili mtazamo wa wageni kuhusu China na wachina, na kuwafahamisha kwamba utamaduni wa China ni mkubwa na unavutia, na pia ni utamaduni wenye masikilizano, kwa hiyo tunaweza kuishi kwa pamoja, kutimiza maendeleo kwa pamoja na kujitahidi kwa pamoja kuboresha maisha yetu. Halafu nilifikiri kwamba kama nikijiunga nao, pia naweza kutoa mchango wangu."

    Kazi ya kujitolea katika nchi za nje pia imewafundisha wanafunzi hao vijana mambo mengi, kuwafanya wawe na uzoefu wa kuishi kwa kujitegemea, kupanua upeo wao na kuongeza hisia zao za uzalendo na kujivunia taifa lao. Li Ruihong ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha kilimo cha mkoa wa Zhejiang, anasema,

    "Ukiwa ng'ambo, utaweza tu kuwa na hisia za uzalendo na kujivunia taifa ambazo ni tofauti na unazosikia ukiwa nyumbani. Kulikuwa na mwongozaji mashuhuri wa bendi wa Ulaya mwenye umri wa miaka zaidi ya 70, ambaye nilimfundisha Kichina. Anawaambia mara kwa mara kwamba Kichina ni lugha ya siku zijazo, ni lazima wajifunze, kwani wote wataihitaji katika siku za baadaye. Pia alisema, uchumi wa China na maendeleo ya China havizuiliki. Baada ya kutoka nje, tukawa na hisia halisi ya kujivunia kuwa mchina, ni tofauti na unayohisi nyumbani."

    "Dunia ni kubwa, nataka kuiona", ni msemo maarufu kwenye mtandao wa Internet nchini China, unafaa kabisa kueleza hisia za vijana hao wanaojitolea. Kijana Zhong Haoyang kutoka chuo kikuu cha siasa na sheria cha China anaona, uzoefu wake wa kujitolea kwenye kazi hiyo umempatia mawazo mapya kuhusu mpango wake wa kazi katika siku zijazo.

    "Nilipokuwa nyumbani nilikuwa nawasiliana na marafiki na walimu tu, mambo waliyoniambia yote yanatokana na mazingira ya maisha yao, lakini wengi wao wameishi China tu, kwa hiyo uzoefu wao ni wa ndani tu. Safari hii nimetoka nje nitatumia fursa hii kupanua upeo wangu, nifahamu zaidi mila na desturi, na jamii ya hapa. Katika siku zijazo, huenda sitakuwa kama wanavyotarajia, na kufanya kazi wanazotaka nifanye, katika siku za baadaye huenda nitajiingiza kwenye shughuli za kimataifa."

    Akizungumzia vijana hao wanaojitolea, mkuu wa chuo cha Confucious katika chuo kikuu cha Bucharest Bw. Dong Jingbo anasema,

    "Wote wanaojitolea kufanya kazi hapa ni vijana, na wameonesha sura ya vijana wa China. Kwa kawaida walimu wanaotumwa na serikali wana umri wa miaka 40 hadi 60, wachache tu ni vijana. Ujana ni nguvu yao, na pia ni tofauti yao. Vijana hao wameonesha sura ya vijana wa China, na pia wamejipatia fursa. Hii ni tofuati kubwa kati ya walimu na wanaojitolea."

    Kuna msemo wa kichina unaosema "Kila ifikapo sikukuu, hukumbuka zaidi jamaa na ndugu". Ijumaa iliyopita ilikuwa ni sikukuu ya mwaka mpya, vijana hao wanaojitolea kufundisha lugha ya Kichina nchini Romania pia walitumia fursa hiyo kutoa salamu za heri ya mwaka mpya kwa nchi na jamaa zao. Bw. Li Zhao anayesoma katika chuo kikuu cha Bucharest anasema:

    "Nikiwa mchina naitaka nchi yetu iwe na ustawi zaidi; nikiwa mwalimu anayejitolea wa kufundisha lugha ya kichina, nakitakia mafanikio makubwa chuo cha confucious, kuwafahamisha waromania wengi zaidi kuhusu utamaduni wa China, na kuwafanya wapende na kukubali utamaduni wa China. Binafsi, nawatakia ndugu na jamaa zangu afya njema na mafanikio katika mwaka mpya, pia najitakia mafanikio katika masomo yangu!"

    Mwaka 2015 umepita na mwaka 2016 umeanza. Wakati kengele ya mwaka mpya ilipokuwa ikilia, vijana hao wanaojitolea kueneza utamaduni wa China walisherehekea kwa pamoja sikukuu ya Mwaka mpya. Kupitia shauku na uchangamfu wao, tunaweza kujua kwamba uzoefu wa kazi hiyo ya kujitolea utakuwa kumbukumbu isiyosahaulika kwenye maisha yao. Kwa kutumia fursa hii, pia tunawatakia vijana hao kila la heri katika mwaka mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako