• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa ukanda wa kiuchumi wa njia hariri wasaidia nchi za Mashariki ya Kati kufufua uchumi na kulinda utulivu wa kikanda

    (GMT+08:00) 2016-01-15 10:10:13

    Naibu mkurugenzi wa taasisi ya uhusiano wa kimataifa wa kisasa ya China Bw. Li Shaoxian amesema ujenzi wa ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri na njia ya hariri baharini ya karne ya 21, utazisaidia nchi za Mashariki ya Kati kufufua uchumi na kulinda utulivu wa kikanda.

    Bw, Li amesema kwa sasa eneo la Mashariki ya Kati liko katika kipindi cha kupanga tena ramani ya kisiasa, kubadilisha miundo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, na kurudisha uwiano kati ya makundi mbalimbali ya kisiasa, hivyo misukosuko inatokea mara kwa mara. Katika hali hii yenye utatanishi, China inatoa mchango mkubwa katika utatuzi wa masuala ya kanda hiyo. Ujenzi wa ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri na njia ya hariri baharini ya karne ya 21 unaohimizwa na China, utasaidia uchumi wa kanda hiyo kufufuka na kuwa tulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako