• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IAEA yasema Iran imeanza kutekeleza makubaliano ya nyuklia

    (GMT+08:00) 2016-01-17 17:09:57

    Ripoti iliyotolewa tarehe 16 na Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA imethibitisha kuwa Iran imeanza kutekeleza makubaliano kuhusu suala la nyuklia la Iran.

    Mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano jana huko Vienna ametangaza kuwa, ripoti ya shirika hilo limethibitisha kuwa Iran imekamilisha hatua zote za maandalizi ya kutekeleza makubaliano ya nyuklia, hali inayomaanisha kuwa makubaliano hayo yataanza kutekelezwa rasmi siku hiyo, na jumuiya ya kimataifa inaondoa vikwazo dhidi ya Iran.

    Mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za diplomasia na usalama Frederica Mogherini na waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammed Javad Zarif pia walitoa taarifa kwa nyakati tofauti kuwa kutokana na uthibitisho wa ripoti ya IAEA, vikwazo vya kiuchumi na kifedha dhidi ya Iran vitaondolewa siku hiyo kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa.

    Naye waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry pia amethibitisha kuwa Iran imetimiza ahadi zake, na kusema kuwa kutokana na hatua zilizochukuliwa baada ya kufikia makubaliano, dunia ya sasa imekuwa salama zaidi kwa kuwa matishio ya silaha za nyuklia yamepungua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako