• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping kufanya nchini Saudi Arabia, Misri na Iran

    (GMT+08:00) 2016-01-18 10:27:42

    Rais Xi Jinping wa China kuanzia tarehe 19 hadi 23 mwezi huu atafanya ziara katika nchi tatu za Mashariki ya Kati, Saudi Arabia, Misri na Iran. Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Xi nje ya nchi kwa mwaka huu.

    Balozi wa China nchini Saudi Arabia Bw. Li Chengwen amesema, lengo la ziara ya rais Xi nchini Saudi Arabia ni kuinua uhusiano wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Rais Xi atakutana na viongozi wa Saudi Arabia na kupanga kwa pamoja maendeleo ya hatua ijayo kuhusu uhusiano kati ya nchi zao.

    Balozi wa China nchini Misri Bw. Song Aiguo amesema, nchini Misri, Rais Xi na viongozi wa nchi hiyo watajadili masuala muhimu kuhusu uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili, ikiwemo kuzidisha uhusiano wa kisiasa kati ya nchi mbili, kuinua kiwango cha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, na kuimarisha mawasiliano ya kirafiki kati ya nchi mbili.

    Balozi wa China nchini Iran Bw. Pang Sen amesema, ziara ya rais Xi nchini Iran ina lengo la kujibu ziara ya rais Hassan Rouhani nchini China mwezi wa Mei mwaka jana, na ni hatua muhimu ya kudumisha mawasiliano ya kisiasa kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako