• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais wa China Mashariki ya Kati kuongeza nguvu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili

    (GMT+08:00) 2016-01-18 18:47:35

    Rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kufanya ziara katika nchi za Saudi Arabia, Iran, na Misri kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 23 mwezi huu.

    Akizungumzia ziara hiyo, naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhang Ming leo amesema, ziara hiyo ina umuhimu mkubwa kwa uhusiano kati ya China na nchi hizo tatu. Bw. Zhang Ming amesema wakati rais Xi Jinping akiwa nchini Misri, atatembelea makao makuu ya Umoja wa nchi za kiarabu, na kueleza sera ya China ya kuhimiza amani na maendeleo ya Mashariki ya Kati, na kutoa mapendekezo na hatua halisi za ushirikiano kati ya China na nchi za Mashariki ya Kati.

    "Hali ya mashariki ya kati inaathiri dunia nzima. Kama hali ya huko itakuwa tete, huenda dunia nzima haitakuwa na utulivu. China inaunga mkono kithabiti nchi za kanda hiyo kutafuta njia za kujiendeleza zinazoendana na hali zao. China inapendekeza kujenga Mashariki ya Kati yenye maendeleo, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi kuisaidia kanda hiyo kujiendeleza kiuchumi na kijamii. Vilevile China inapendekeza kujenga Mashariki ya Kati yenye usalama, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kufuata katiba ya Umoja wa Mataifa na kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa na kuziunga mkono pande mbalimbali zinazohusiana na masuala nyeti ya kanda hiyo kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo. "

    Habari nyigine zinasema, kabla ya kufanya ziara nchini Saudi Arabia, rais Xi Jinping wa China ameandika makala ya "kuwa wenzi wanaoendelea kwa pamoja" katika gazeti la al Riyadh la nchi hiyo. Katika makala hiyo, rais Xi amesema, Saudi Arabia ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya mwaka 2016, na pia ni nchi ya kwanza ya kiarabu anayozuru baada ya kuwa rais wa China. Anatarajia kuwa kupitia ziara hiyo, atashirikiana na viongozi wa Saudi Arabia kuinua kiwango cha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo kufikia ngazi mpya na kunufaisha wananchi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako