• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi ana matumaini na ukuaji wa Uchumi

    (GMT+08:00) 2016-01-19 10:34:12

    Licha ya shinikizo linalotokana na kushuka kwa ongezeko la uchumi wa China na hali tete kwenye soko la fedha, hivi karibuni Rais Xi Jinping wa China amesema msingi wa uchumi na mipango ya muda mrefu ya China bado ni thabiti.

    Rais Xi aliyasema hayo katika kongamano lililohudhuriwa na mawaziri na viongozi wa mikoa na kuongeza kuwa hali mpya ya kawaida ya kiuchumi itajitokeza wakati wa awamu ya 13 ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

    Rais Xi amesema wakati uchumi ukikua, kiwango cha ukuaji kitakuwa cha wastani, hivyo muundo wake ni lazima ubadilike na kuwa na njia mpya za ukuaji. Uchumi wa China umeongezeka kwa asilimia 6.9 katika robo ya tatu ya mwaka 2015, ikiwa ni pungufu kidogo kutoka asilimia 7 katika robo ya pili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako